KUJENGWA KWA AL-KA'AB ZAMA ZA MTUME ﷺ
Baada ya muda wa miaka thalathini na tano tokea kuzaliwa kwa Mtume ﷺ, Makuraishi walisimama katika ujenzi wa Al-Ka'aba. Jambo hili lilifanyika kwa sababu Al-Ka' aba ni jengo la mawe lenye urefu wa mita 6.30 tokea zama za Ismail na haikuwa na kiezeko na kwa sababu hiyo kundi la wezi liliwahi kuiba mali iliyokuwa ndani ya Al-Ka'aba. Jengo lake lilikuwa limeanza kupatwa na udhaifu kwa kuchakaa,hasa ikizingatiwa kuwa ilikuwa ni nyumba ya kale. llipatwa na udhaifu huo kutokana na ukale na zikapasuka kuta zake.
Kabla ya kupewa kwake Utume kwa miaka mitano mji wa Makka ulikumbwa na mafuriko makubwa sana yaliyoporomokea kwenye nyumba tukufu ya Al-Ka'aba.Kutokana na mafuriko hayo Al-Ka'aba ilikaribia kubomoka kabisa. Makuraishi walilazimika kulijenga upya jengo lake ili kuirudisha hadhi yake. Katika hili walikubaliana wote kuwa isiingie katika ujenzi huo isipokuwa mali ya halali, kwa hiyo hawataingiza mali yenye kutokana na zinaa, wala mauzo ya riba, wala mali iliyopatikana kwa njia ya dhuluma.
Wakati wa kuanza ujenzi ulipofika wakawa wanaogopa kuibomoa Al-Kaaba, mpaka alipoanza kuibomoa Al-Walid ibn Al-Mughirah Al-Makhzumi, ndio na watu wengine wakamfuata baada ya kuona kuwa hakupatwa na jambo lolote. Walibomoa mpaka walipofika katika misingi iliyojengwa na Ibrahim (a.s). Walipotaka. kuanza ujenzi,wakaigawa Al-Ka'aba na kulihusisha kila kabila sehemu yake,wakaanza kuijenga na msimamizi wa ujenzi huo alikuwa Mrumi aliyekuwa akiitwa Baqum, jengo lilipofika mahali pakuwekwa jiwe jeusi, walitofautiana ni nani ambaye atapwekeka kwa kupata utukufu wa kuliweka mahali pake.
Siratu Ibn Hisham, [uzuu 2, Uk. 162-197.
104 Ibn Hisham, Juzuu I, Uk. 128.
Arraheeq Al Makhtum 94-96
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.