KUMUOA BIBI KHADIJA
Mtume ﷺ Aliporudi Makka Bi Khadija aliona mambo ambayo hajapata kuyaona kabla ya hapo, katika kuongezeka mali yake. Uaminifu wa Mtume na baraka zake ulikuwa wazi kwake. Ukichanganya na aliyoelezwa na kijana wake Maysara katika yale ambayo aliyaona kwa Mtume ﷺ miongoni mwa mambo mazuri, sifa bora, fikra nzuri, kauli za ukweli, na uaminifu, Bi Khadija alikuwa amepata kile alichokuwa anakitaka.
Kabla ya hapo mabwana na viongozi mbalimbali walikuwa wakifanya hima kutaka kumwoa, naye aliwakatalia jambe hilo. Bi Khadija aliyaeleza yale yaliyokuwa katika nafsi yake kwa rafiki yake Nafisa binti Miniyah, Rafiki yake huyu alikwenda kwa Mtume ﷺ na akamwomba amwoe BiKhadija, naye akaliridhia jambo hilo.
Mtume ﷺ akawaeleza ammi zake. Wakatoka na kwenda kwa ammi wa Khadija, wakamposa. Baada ya hapo ndoa ilifungwa Ndoa. ilihudhuriwa na Banu Hashim na viongozi wa ukoo wa Mudhar, na jambe hili lilifanyika baada ya kurejea kwake kutoka Syria kwa muda wa miezi miwili na . alilipa mahari yake ngamia ishirini.
Wakati huo Bi Khadija alikuwa na umri wa miaka arobaini, alikuwa mbora wa wanawake katika jamaa zake,kwa nasabu, utajiri na akili. Naye ndiye mwanamke wa kwanza aliyeolewa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ na hakuoa mwanamke mwingine mpaka Khadija alipofariki dunia.
Watoto wake Mtume ﷺ wote walizaliwa na Khadija, isipokuwa Ibrahim.
Kwanza alimzaa Al-Qassim, na kwa Al-Qassim alikuwa akiitwa Abul Qassim, baba wa Qassim. Kisha akazaliwa Zainab, Ruqayya, Ummu Kulthum, Fatma na Abdillahi ambaye pia aliitwa Al-Tai'ib na Al-Tahir.
Walikufa watoto wake wote wanaume katika utoto wao, ama katika watoto wake wa kike, wote waliuwahi Uislamu, wakasilimu na wakahajir kwenda Madina. Wote walifariki katika uhai wa Mtume ﷺ, isipokuwa Bibi Fatma ambae alifariki baada ya miezi sita ya kifo cha Mtume ﷺ.*
* lbn Hisham, Juzuu 1, Uk. 189-190. Al-Ghazali, Fiqhi Sira, Uk. 59. Tnlqiyh
Fuhum Ahlul Athar, Uk. 7.
Arraheeq Al Makhtuum 93
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.