TUMERIDHIKA NA AL-AMIIN
Mzozo uliendelea kwa muda wa siku nne au tano hivi na ukazidi mpaka kufikia hatua ya kutaka kuzusha vita kubwa kabisa katika ardhi tukufu. Ilipofikia, hali hiyo Umayya bin Mughiira Al-Makhzumi alipendekeza kwao kuwa ipo haja ya kumtafuta msuluhishi wa kuupatia ufumbuzi mzozo uliotokea kati yao.
Wakakubaliana na ikapemfekezwa kuwa mtu wa kwanza atakaeingia hapo kupitia mlango wa msikiti ambao wote waliuridhia ndiye atakayekuwa msuluhishi wao.Mwenyezi Mungu ﷻ Akataka mtu huyo awe ni Mjumbe Wake Mwenyewe. Walipomwona walipiga kelele kwa furaha na kusema: 'Huyu ni mtu mwaminifu, tumemridhia.
Muhammad ﷺ alipofika pale walipokuwa, walimweleza khabari zao, baada ya kuwasikiliza aliomba kishali kutoka kwa mmoja wao na akaliweka lile jiwe katikati yake,akawataka viongozi wa makabila husika kila mmoja akamate ncha ya kishali na akawaamrisha walinyanyue mpaka walipolifikisha mahali pake, yeye akalichukua kwa mkono wake na kuliweka mahali pake na huu ukawa ni ufumbuzi wa busara sana ambao waliuridhia wote.
Makuraishi walipungukiwa na mali ya halali,wakalazimika kutoa kiasi cha yadi sita sehemu ya Kaskazini na hiyo ndiyo sehemu inayoitwa Hijr na Al-Hatim na waliunyanyua mlango wake kuuepusha na usawa wa ardhi,ili asije akaingia Al-Ka'aba isipokuwa yule.wanaemtaka. Jengo lilipofika kiasi cha urefu wa yadi kumi na tano, waliliinua paa kwa nguzo sita.
Baada ya kwisha kwake Al-Ka'aba ikawa na umbile la pembe nne, urefu wa nguzo zake ulikuwa ni mita kumi na tano (15) ambayo iko katika jiwe jeusi na ile inayokabiliana nayo ni mita kumi 10 kila moja. Jiwe jeusi liliwekwa kiasi cha urefu wa mita 1.50 kutoka katika ardhi tukufu; na inazungukwa na nguzo ambayo iko mlangoni na ile ambayo inakabiliana nayo ni kiasi cha mita kumi na mbili (12) kila moja. Mlango wake ulikuwa na urefu wa mita mbili juu ya ardhi. Kinaizunguka hiyo AI-Ka' aba kwa upande wa nje kitu chenye uwazi kwa ndani, katika jengo kwa chini yake kuna ukuta, urefu wake ni mita 0.25 na upana wake ni mita 0.30, na kitu hicho chenye uwazi kwa ndani kinaitwa As-Shadharwan,kitu hicho chenye uwazi kwa ndani kinaitwa As-Shadharwan,na hicho ni katika msingi wa Al-Ka'aba isipokuwa Makuraishi waliuacha.
Siratu Ibn Hisham, [uzuu 2, Uk. 162-197.
104 Ibn Hisham, Juzuu I, Uk. 128.
Arraheeq Al Makhtum 96
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.