SAFARI YA KWENDA SHAM KWA AJILI YA BIASHARA
Alipofikisha umri wa miaka ishirini na tano, alitoka kuelekea Sham kwa madhumuni ya kufanya biashara katika mali ya Bi Khadija (r.a). Ibn Ishaq anasema: 'Bi khadija binti Khuwaylid alikuwa ni mwanamke mfanyabiashara mtukufu, aliyekuwa na mali nyingi, alikuwa akiwakodisha wanaume kutoka katika mali yake, alikuwa akiwapa mali yake waifanyie biashara kwa kuwapa kitu kutoka katika faida itakayopatikana. Shughuli kubwa za Makuraishi wakati huo ilikuwa ni kufanya biashara.
Bi Khadija alipopata khabari za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ, kuhusu tabia ya ukweli katika mazungumzo yake, wingi wa uaminifu wake na ubora wa tabia zake,alipeleka ujumbe kwake akimuomba atoke na mali yake kuelekea Syria kwa madhumuni ya kufanya biashara na kwamba atampa malipo bora kabisa zaidi ya vile anavyofanya kwa wafanya biashara wengine. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ alilikubali wazo hilo, akatoka na mali za Bi Khadija kuelekea Syria, akifuatana na kijana wake Bi Khadija aitwae Maysara.(1)
1) Ibnu Hisham, Juzuu 1, Uk. 187-188
Ar-raheeq Al Makhtum. 92
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.