KIAPO CHA AL-FUDHUUL
Baada ya vita hivi ulipatikana rmkataba wa AI-Fudhoul katika mwezi wa Dhul-Qaada (mfungo pili) wakati wa mwezi mtukufu. Katika mkataba huu yaliitana makabila ya Makuraishi, Banu Hashiin, Banu Al-Muttwalib, Assad bin Abdil-Uzza, Zuhra bin Kilab na Taym bin Murrah,walikutanika katika nyumba ya Abdillahi Bin Jadaan Al- Ti'm. Kwa sababu ya umri wake na utukufu wake, wakafanyiana mkataba na kuahidiana kuwa kusiwepo katika mji wa Makka mtu aliyedhulumiwa, na kati ya watu wa Makka na watu wengine pia wanaokuja Makka kwa shughuli mbalimbali. Walikubaliana kuwa ikitokea hivyo watasimama pamoja na mtu huyo dhidi ya aliyemdhulumu mpaka amrudishie haki yake.
Mkataba huu ulishuhudiwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ naalisema baada ya kutukuzwa na Mwenyezi Mungu ﷻ kwa Utume:
لقد شهدت مع عمومتي حلفا في دار عبد الله بن جدعان، ما أحبّ أن لي به حمر النعم ولو دعيت به في الإسلام لأجبت] رواه أحمد]
[Kuia hakika nimeshuhudia pamoja na Maami zangu Mkataba mzuri katika nyumba ya Abdillahi Bin Jada'an. Lilikuwa ni jambo zuri kwangu kuliko kupetoa ngamia mia moja wekundu na lau ningealikwa kuhudhuria mkaiaba wa aina hiyo kaiika Uislamu ningeitika.] [Imepokewa na Ahmad]
Madhumuni na msingi wa mkataba huu unapingana na majivuno, jeuri na ari ya koo na ukabila iliokuwepo wakati wa Jahiliyyah. Inasemekana kuwa miongoni mwa sababu za mkataba huu ni kuwa mtu mmoja kutoka katika ukoo wa Zubaid alifika Makka akiwa na bidhaa akiuza na bidhaa hizo zikanunuliwa na Al-' As bin Wa'il As-Sahmy. Bwana huyu akamzuilia haki yake, akawahamasisha marafiki zake Abdi-Ad-Dar Makhzoum, Jum'ah, Saham na' 'Adi, ambao hawakumjali" akapanda mlima wa Abu Qubais, akatoa wito kwa kuyatumia mashairi., ndani yake akielezea kudhulumiwa kwake, hali ya kuyanyua sauti yake. Katika kuisikiliza sauti hiyo alijitokeza Al-Zubair bin Abdul Muttwalib akasema; Anaamini huyu kuwa ameachwa (hakuna wa kumsaidia)?" Walikusanyika wale ambao umepita utajo wao- katika Mkataba wa Al-Fudhoul, wakatoka na kwenda kwa Al-' Asi bin Wa'il wakachukua kwa nguvu kutoka kwake haki ya Al- Zubaid baada ya kumwonyesha mkataba. 1*
1) Arraheeq Al Makhtum 91
Ibn Hisham, Juzuu I, Uk. 66.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.