VITA VYA AL-FIJAR
Wakati Mtume ﷺ alipofikisha umri wa miaka kumi na mitano vilitokea vita vya Al-Fijar kati ya Makuraishi na wale waliokuwa pamoja nao miongoni mwa Kinana, na Qais 'Ailan. Kiongozi wa Makuraishi na Kinana alikuwa ni Harb Bin Umayya, kwa sababu ya cheo chake kwao, kwa umri na utukufu. Ushindi ulikuwa ni wa Qais dhidi ya Kinana, mpaka ilipofika katikati ya mchana ushindi ulikuwa ni wa Kinana dhidi ya Qais. Vita hivi viliitwa kwa jina la Al-Fijar, kwa sababu ya kuvunjwa kwa mambo matukufu ya Al-Haram na miezi mitukufu. Vita hivi vilihudhuriwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ na alikuwa akikusanya mikuki na mishale ya maadui na kuwapa ammi zake waitumie." 1*
1) Arraheeq Al Makhtum 89
* Mukhmear Siratu Rrasul, Uk. 16. Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 180-183.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.