KUKUTANA NA MTAWA (ARRAHIB) BAHIRA
Wakati Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ alipofikisha miaka kumi na miwili, pamesemwa kuwa na miezi miwili na siku kumi, Abi Twalib alisafiri naye katika safari zake za kibiashara kwenda Sham, alikwenda mpaka akafika Basra Basra wakati huo ikihesabiwa kuwa ni katika Sham na mji Mkuu wa nchi ya utawala wa Warumi.Katika mji huu, enzi hizo kulikuwepo na mtawa aliyekuwa akijulikana kwa jina la Bahira. Jina lake halisi alikuwa akiitwa Jarsis. Msafara ulipofika alitoka akawakaribisha na kuwakirimu kama wageni wake. Kabla ya hapo alikuwa hajawahi kufanya jambo hilo. Bahira alikuwa amemtambua Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ kwa sifa zake, akasema na hali ya kuwa amemkamata mkono wake (Muhammad ﷺ)
{هَذَا سَيِّدُ الْعَالَمِين, هَذَا يَبْعَثُهُ اللَّهُ رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ}
"Huyu ni Bwana wa walimwengu, Mwenyezi Mungu ﷻ Atampa ujumbe hali ya kuwa ni rehema kwa walimwengu wote."
Abi Twalib akamuuliza: 'Ni jambo gani lililokufahamisha hivyo?' Akajibiwa: 'Kwa hakika wakati nyinyi mlipolikaribia Jabali halikubaki jiwe lolote wala mti wowote isipokuwa ulipomoka kwa kusujudu, na havisujudu vitu hivi isipokuwa ni kwa Mitume tu.
Mimi ninamuelewa huyu kwa muhuri wa mwisho wa Utume, ambao uko chini ya mfupa laini wa bega lake, mfano wa tufaha; na sisi tumezikuta khabari zake katika vitabu vyetu.
Akamuomba Abi Twalib amrudishe Makka na asiende naye Sham, kwa kuwahofu Mayahudi waliokuwa huko, akawaamuru ammi yake pamoja na watoto wake warejee, Makka.*
* Arraheeq Al Makhtuum Uk. 89
Mukhmear Siratu Rrasul, Uk. 16. Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 180-183. Katika
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.