KULELEWA NA AMMI YAKE ABUU TWALIB
Alipofariki Babu yake Mtume ﷺ, Abi Twalib alichukua jukumu la kumlea mtoto wa ndugu yake kwa njia iliyo kamilifu kabisa, alimkusanya pamoja na watoto wake, akamfadhilisha mbele yao, akampa ziada ya heshima na utukuzo, Aliendelea kwa muda wa miaka arubaini akimuhami na akimkunjulia himaya yake, akafanya urafiki na watu na akagombana nao kwa ajili yake. Kwa ufupi ni kuwa mahusiano ya ammi yake Abi Twalib na watu wengine yalikuwa ni mazuri pindi watu wale watakapokuwa na uhusiano mzuri na Muhammad ﷺ.
KUOMBWA MVUA KUPITIA DHATI YAKE
Ibni Assakir amethibitisha kutoka kwa Jalhamah bin Urfata ambaye amesema; 'Nilifika Makka wakati watu wakiwa katika hali ya ukame, Makuraishi wakasema: 'Ewe Abi Twalib jangwa limekuwa na ukame, watu wamekuwa na njaa, njoo uombe mvua.' Akatoka Abi Twalib akiwa pamoja naye kijana, kana kwamba kijana huyo ni jua lilIkrfunikwa na mawingu, kikatanzuka kwake kiwingu chenye kheri, pembezoni mwake wapo vijana wadogo wadogoi Abi Twalib akamchukua, akauambatisha mgongo wake na Al-Ka'aba, akikandamiza kidole chake kwa yule kijana na hali yakuwa mbinguni hakuna kipande cha wingu, ghafla yakazuka mawingu kutoka huku na huko na ikanyesha mvua na ikamimina maji viungani. Kwenye hili ameashiria Abi Twalib wakati aliposema:
وأبيض يستسقى الغمام بوجهه ** ثِمال اليتامى عصمة للأرامل
يلوذ به الهلاك من آل هاشم ** فهم عنده في نعمة وفواضل
*Arraheeq Al Makhtuum Uk. 88
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.