KUFARIKI KWA MAMA YAKE MWENYE HURUMA SANA
Baada ya tukio hili, Halima alipata hofu juu ya maisha ya Mtume ﷺ na akaamua kumrudisha kwa mama yake. Akawa chini ya uangalizi wa mama yake mpaka alipofikisha umri wa miaka sita
Katika kuadhimisha kumbukumbu ya mume wake aliyekufa Bi Amina aliamua kuzuru kaburi lake huko Yathrib, umbali wake unafikia kilometa mia tano.Akatoka Makka akiwa pamoja na mtoto wake yatima - Muhammad ﷺ - na mtumishi wake Ummu Ayman, na msimamizi wake Abdul Muttwalib. Akakaa huko kwa muda wa mwezi mmoja kisha akaamua kurejea. Wakati wakiwa njiani kurejea Makka ghafla alipatwa na maradhi, maradhi yakamzidi na akafariki dunia huko Abwaa, kati ya Makka na Madina.*
* Arraheeq Al Makhtuum 85
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.