Menu

KABILA LA KURAISHI NA UTAWALA WAKE


QURAYSH


Makabila mengi yalipatikana kutokana na kizazi cha Ismail mwana wa Nabii Ibrahimu katika nchi ya Hijazi, kabila la Qurayshi ndilo lililokuwa mashuhuri zaidi.

Baadhi ya makabila haya yalikuwa yakimuabudu Mwenyezi Mungu kupitia mafundisho ya dini ya Nabii Ibrahim- Amani ya Allah imshukie.

Uongozi wa kidini na kibiashara ulitawaliwa na Maqurayshi kwa sababu ya ushujaa na ufasaha waliokuwa nao, sifa hizi ndizo zilizolipelekea kabila la Qurayshi kuyatawala makabila mengine yote.

Mji wa Makkah na Maqurayshi walizidi kupata utukufu pale Mzee Qusway Bin Kilaab-babu wa nne wa Mtume aliposhika hatamu za uongozi wa mji wa Makkah.

Mzee huyu alikuwa ni mtu mwenye busara, fikra na hekima. Alianzisha mpango mji, bunge ili watu wote wa Makkah waweze kukutana humo na kushauriana/kujadili mambo yao, pia aliijenga upya Al-Kaaba baada ya kuanza kuonyesha athari za kubomoka.

Kadhalika alianzisha utaratibu wa kuwasaidia masikini kwa kuwapa chakula na maji. Baada ya kupita vizazi vingi, taratibu Maqurayshi walianza kuyatupa mafundisho ya dini ya Nabii Ibrahimu na kuanza kuyaabudu masanamu yaliyotengenezwa na mikono yao wenyewe.

Ibada ya msanamu ilikuwa ni matokeo ya safari ya mmoja wa viongozi wa Maqurayshi Amru bin-l Hayy, Alikuwa ni wakutoka kabila Khuza'a alipokewenda Shamu na kuwakuta watu wa huko wakiyaabudia masanamu na akapendezwa na kuvutiwa na ibada hiyo.

Akarejea Makkah na sanamu moja, akaliweka ndani ya Al-kaaba na kuanza kuliabudia.Na huyu ndie mtu wa kwanza alie leta masanamu na kubadili dini ya Nabii Ibrahim (A.s) ya kuabudiwa Mungu mmoja.

Na Mtume ameeleze mwisho mbaya wa huyu bwana kwa kitendo kibaya alicho kifanya cha kuabudiwa Masanamu badala ya Mwenyezi Mungu.Amesema Mtume:

 

[رأيت عمرو بن لحي يجر قصبه في النار" يعني أمعاءه]

 

[Nimemuona Amru binl-Hayy akikokota tumbo lake katika Moto wa Jahannam]

Watu wa Makkah kuona hivyo nao wakamuiga kiongozi wao, wakatengeneza masanamu yao wakayaweka ndani ya Al-kaaba na kuyaabudia na huo ukawa ndio mwanzo wa kuiacha na kuitupa mila ya Nabii Ibrahimu.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

7887005
TodayToday138
Highest 05-20-2026 : 12580
US
Guests 67

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6a3b7ed14781616328656981782283985
title_6a3b7ed147865980965101782283985
title_6a3b7ed1478b15595531081782283985

NISHATI ZA OFISI

title_6a3b7ed147e6c17755377861782283985
title_6a3b7ed147eb919132389601782283985
title_6a3b7ed147f057639279761782283985 Add content here

HUDUMA MPYA

: 11 + 11 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com