Menu

NASABA YA MTUME KWA UPANDE WA MAMA YAKE


mqdefault 2


Nasabu yake Bwana Mtume kwa upande wa mama yake:-

Mama yake ni:  Aaminah Bint Wahab Bin Abdi Manaf Bin Zuhrah Bin Hakiym.

Huyu Mzee Hakiym ndiye Kilaab ambaye ni babu wa tano wa Mtume kwa upande wa baba yake.

Tumekwishaeleza huko nyuma kwamba huyu Mzee Qusway ambaye ni babu wa nne katika

mlolongo wa babu zake Mtume ndiye aliyeweka mpango wa mji wa Makkah na akawaunganisha pamoja Waarabu kwa kuondosha ukabila.

Baada ya kifo cha Mzee Qusway, hatamu za uongozi wa mji wa Makkah zilishikwa na babu wa pili wa Mtume Mzee Haashim. Huyu alikuwa tajiri na ndiye aliyeasisi mfumo wa biashara za Kusi na kaskazi kama ulivyoelezwa na Qur'ani:

 

لِإِيلَافِ قُرَيْشٍ  إِيلَافِهِمْ رِحْلَةَ الشِّتَاءِ وَالصَّيْفِ}    قريش1-2}

 

"ILI KUWAFANYA MAKURESHI WAENDELEE. WAENDELEE NA SAFARI ZAO ZA WAKATI WA KUSI (kwenda yaman) NA WAKATI WA KASKAZI (kwenda Shamu, ndio maana tukajaalia jeshi la ndovu kushindwa) (106:1-2)

Pia Mzee huyu ndiye aliyesimamia usambazaji wa maji na chakula kwa wageni wote wanaokuja kufanya ibada katika Al-kaaba na hili linaashiria ukarimu walikuwa nao Waarabu.

Naye ndiye mtu wa mwanzo aliyeanzisha uokaji na usambaji wa mikate katika mji wa Makkah na hili linaonyesha ni jinsi gani alivyowajibika kwa jamii iliyompa dhamana ya uongozi.

Mwenyezi Mungu aliitakasa nasabu ya Mtume kutokana na uchafu wa kijahilia.

Mababa zake wote walikuwa ni watu watukufu na viongozi kama ambavyo mamama zake pia walikuwa ni wanawake waungwana,watakasifu wasio na uchafu wowote.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668041
TodayToday729
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 14

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68669c122122619976556121751555090
title_68669c12213108441554001751555090
title_68669c12213f611807435721751555090

NISHATI ZA OFISI

title_68669c12229e915233395891751555090
title_68669c1222ac51836088421751555090
title_68669c1222b9b10634934991751555090 Add content here

HUDUMA MPYA

: 8 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com