HALI YA KIJAMII NA TABIA ZA WAARABU
Makabila mengi ya kiarabu yametokana na kizazi cha Nabii Ismail.(A.S)
Kila kabila liliundwa kutokana na kaya/familia kadhaaa zilizojiunga pamoja.
Kila kabila liliongozwa na kiongozi aliyekuwa mtu mzima anayeheshimika, kukubalika na kutiiwa na wote.
Ukabila ulikuwa ndio sera ya kila kabila, na kila kabila lilikuwa tayari kuilinda sera yake hiyo ya ukabila dhidi ya uadui wa wote ule kutoka makabila mengine kwa gharama yoyote ile.
Msimamo huu na sera hii ya ukabila ilisababisha mizozo, ugomvi na mapigano ya mara kwa mara baina ya makabila haya.
Kugombea vyanzo vya maji, machungo na kujifakharisha kwa nasabu pia vilichochea kwa kiasi kikubwa mizozo na mapigano.
Kama ambavyo watu hutofautiana katika vyeo/hadhi, kazi na hali za kimaisha, Waarabu pia waligawanyika katika matabaka yafuatayo:
1. Mabwana/Viongozi: hawa ndio waliokuwa na mamlaka juu ya wengine na hatamu za uongozi zilikuwa chini yao.
2. Makuhani: hawa walikuwa ndio viongozi wa kidini wakiyatawalia mambo yote yanayohusu dini ikiwa ni pamoja na ibada, sherehe za kidini na mengineyo.
3. Wafanyabiashara: hawa walijishughulisha na usambaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya maeneo yao.
4. Wachungaji: hawa ndio waliokuwa wakijishughulisha na uchungaji wa wanyama na kazi ya kilimo kwa kiasi fulani.
Ama kwa upande wa kitabia,Waarabu za jahilia kama walivyo watu wa zama hizi walikuwa na tabia nzuri na nyingine mbaya.
Miongoni mwa tabia njema walizokuwa nazo ni kama vile ukarimu, murua, ushujaa na utekelezaji wa ahadi.
Tabia mbaya zilizoitawala jamii ile ni pamoja na ulevi, uchezaji wa kamari, ulaji riba na kuwazika watoto wa kike wakiwa hai kama ilivyoelezwa na Qur'ani tukufu:
وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ} التكوير:8-9}
"Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,Kwa kosa gani aliuliwa? [81:8-9]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.