Menu

FAIDA ZA KUTAWADHA KIMWILI NA KINAFSI 

 

Suali: Ni ipi faida ya kutwadha kinafsi na kimwili ??

Jawabu: kwanza kabisa ni lazima kujua kuwa kutawadha ni ibaada tukufu Mwenyzi Mungu (Subhanahu wata'ala ) ameamrisha wakati mtu anapo taka kuswali. Na lizima afute Mamrisho ya allah sawa atakuwa ni mwenye kujua hikma yake au asijue,na bila shaka katika kutawadha kuna hikama na kuna faida ambazo Mwenyezi mungu ndie anaejua sawa tuzijue au tusizijue,na katika faida ya kutawadha kinafsi ni kuwa mtu kutawadha wakati akiwa na hasira hushusha hasira zake,kama ilivyo kuja kwenye Hadithi


عن عقبة بن محمد السعدي عن أبيه عن جده أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: إن الغضب من الشيطان، وإن الشيطان خلق من النار، وإنما تطفأ النار بالماء، فإذا غضب أحدكم فليتوضأ.  والحديث أخرجه الإمام أحمد

Amepokea Uqbah bin Muhammad kutoka kwa babake kutoka kwa babu yeke,kwamba Mtume rehma na amani zimfikie yeye amesema [hakika hasira hutokamana na Shetwani, na shetwani ameumbwa kwa Moto,na Moto hizimwa kwa maji,basi atakapo kasirika Mmoja wenu natawadhi]  Imepokewa na Imam Ahmad,lakini hadithi Amedhofishwa na Sheikh Al-Albaniy Mungu amrehemu.
Na katika faida ya kutawdha kimwili,ni kuwa huupa mwili nishati,kwa dalili kuwa Mtume rehma na amani zimfikie amearish kwa Yule alie muingilia mkewe na akataka kurudi tena kumuingilia akatawadhe, kama ilivyo kuja katika Hadithi ilio pokelewa na Imam Muslim:


"إ ذا أتى أحدكم أهله ثم أراد أن يعود فليتوضأ."
  

[Atakapo muingilia Mmoja wenu mkewe kasha akataka kurudi (kutaka kumuingilia tena) basi Akatawadhi]

Na katika riwaya ya Ibn Hibbani imekuja kwa matamshi haya:


"إذا أتى أحدكم أهله ثم أراد أن يعود فليتوضأ فإنه أنشط للعود." 

[Atakapo muingilia Mmoja wenu mkewe kasha akataka kurudi basi akatawadhe kwani atarudi na shiti]
Na kutawadha huku japo kuwa silazima,lakini kuna dalili yakuwa kutawadha huupa mwili nishati,hizi ni badhi ya faida ya kutawadha kimwili na kinafsi na bila shaka kuna faida nyingi kwani katika Mamrisho yake allah hapakosekani faida kwa Mwanadamu sawa awe ni mwenye kuzijua  au asiwe ni mwenye kuzijua.

Na Allah ndie mjuzi zaid


 

 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668038
TodayToday726
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 8

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68669c122122619976556121751555090
title_68669c12213108441554001751555090
title_68669c12213f611807435721751555090

NISHATI ZA OFISI

title_68669c12229e915233395891751555090
title_68669c1222ac51836088421751555090
title_68669c1222b9b10634934991751555090 Add content here

HUDUMA MPYA

: 12 + 10 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com