HUKMU YA MTU ALIE KULA NA KUNYWA AKIDHANI KUWA BADO NI USIKU
Suali :
Al fajiri ya siki ya kwanza ya mwezi wa Ramadhan aliniamsha mke wangu akasema jee unataka kunywa maji ? Na nilipochukua maji kutoka kwake nilimuuliza jee kumeadhiniwa ? Akasema :hapana na baada ya kunywa maji kwa dakika 15 - 20 swala ikakimiwa, kwahivyo nikinywa maji baada ya adhana kwa dakika 5 - 10 jee nina makosa ?
Jawabu :
Alhamdulillah kwa hakika wamekhtalifiana wanazuoni kuhusu hukmu ya aliyekula au kunywa akidhania kwamba bado ni usiku na bado Al fajiri haijaingia, na vile vile aliyekula au kunywa akidhania kuzama kwa jua kisha ikambainikia kosa lake.
Wanazuoni wengi wanaona yakwamba Saumu yake inaharibika kwa hilo, na inamlazimu yeye kufunga siku moja badala yake.
Na wanaona wanazuoni wengine yakwamba funga yake ni sahihi na yakwamba yeye atakamilisha funga yake wala hatolipa siku ile aliyokula.
Nayo ni kauli ya Mujahid na Hassan na Twaabiiy, na mapokezi kutoka kwa Imam Ahmad , na amechagua rai hii Al Muzany katika wanazuoni wa madhehebu ya Imam Shafii , na Sheykhul Islam Ibnu Taymiyah na ameipitisha rai hii Sheikh Muhammad Swaleh Al Othaimeen. - Allah awarehemu wote.
Amesema Sheykhul Islam Ibnu taymiyah :
"Na wale wanaosema hajafungua katika zote (yaani : akikosea au kusahau mwanzo wa mchana au mwisho wake ) wamesema hoja yetu ndio yenye nguvu zaidi, na dalili ya Kitabu na Sunna juu ya kauli yetu iko wazi zaidi :
kwani Mwenyzi Mungu alietukuka anasema:
{ربنا لا تؤاخذنا إن نسينا أو أخطأنا}
[Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea.] kakusanya baina ya kusahau na kukosea, na kwa sababu atakayefanya yasiyofaa katika Hijja na katika Swala kwa makosa ni kama aliefanya kwa kusahau , na imethibiti katika Sahihi (AlBukhari) yakwamba Maswahaba walifuturu katika zama za Mtume ﷺ kisha jua likachomoza, na hawakutaja katika hadithi yakwamba wao waliamrishwa kulipa, lakini Hishaam bin Urwah amesema: ni lazima kulipa, na baba yake ni mjuzi kumshinda lakini alikua akisema: Hawalazimiki kulipa na imethibiti katika Sahihi mbili (Bukhari na Muslim)
yakwamba kikundi katika maswahaba walikua wanakula mpaka imdhihirikie mmoja wao uzi mweupe kutokana na uzi nyeusi, na akasema Mtume rehma na amani ziwe juu yake
kumwambia mmoja wao hakika
[إن وسادك لعريض ، إنما ذلك بياض النهار وسواد الليل]
[Hakika Mto wako ni mpana, makusudio ya hilo ni uweupe wa mchana na na uweusi wa usiku]
Wala haijanukuliwa kwamba Mtume ﷺ aliwaamrisha kulipa, na hawa walikua wajinga wa hukumu hivyo basi wakakosea, na imethibiti kutoka kwa Umar bin Al Khatwab yakwamba yeye alifungua kisha ikabainika mchana akasema : "hatulipi kwani sisi hatujakusudia dhambi"; na imepokelewa kutoka kwake yakwamba alisema: "tunalipa" , lakini isnadi ya kwanza ndio iliyothibiti zaidi , na imeswihi kutoka kwake yakwamba yeye alisema: "hili ni jambo dogo"; basi wakatafsiri hilo wenye kutafsiri yakwamba yeye alikusudia kuwa hilo la kulipa saumu ni jambo dogo, lakini lafdhi hii haiashirii hilo .
Kwa ujumla : kauli hii (ya kutolipa) ndio yenye athari kubwa na nadharia yenye nguvu zaidi, na zaidi na Dalili ya Kitabu , Sunna , na kiasi."
Majmuul Fataawa ( 20 / 572 , 573 ) .
Na angalia pia Al Sharhul Mumti ( 6 / 411 )
Na hivyo basi inadhihirika nguvu za dalili za kauli yakwamba Funga yake ni sahihi na wala
hatolipa .
Pamoja na hivyo lau Muislamu atataka kujitoa kwenye shaka na akalipa siku moja mahala pake basi atakua amefanya vizuri .
Na ALLAH ni mjuzi zaidi .
Chanzo: Tovuti ya Fatwa Suali wa Jawabu
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.