KINGA YA MUISLAMU
اللهم اغفر له وارحمه، وعافه ،واعف عنه ،وأكرم نُزُله ، ووسع مُدخلهُ ، واغسله بالماء والثلج والبرد ، ونقه من الخطايا كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس ، وأبدله داراً خيراً من داره ، وأهلاً خيراً من أهله وزوجاً خيراً من زوجه، وأدخله الجنة ،وأعذه من عذاب القبر ( ومن عذاب النار
مسلم 2/663
[Ewe Mwenyezi Mungu msamehe na umrehemu na umuafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake (kaburini) na upanue kuingia kwake, na muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama unavyoitakasa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na muingize peponi na mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto).] [Imepokewa na Muslim.]
اللهم اغفر لحينا وميتنا ، وشاهدنا وغائبنا ، وصغيرنا وكبيرنا ، وذكرنا وأُنثانا ، اللهم من أحييته منا فأحيه على الإسلام ، ومن توفيته منا فتوفه على الإيمان اللهم لا تحرمنا أجره ولا تضلنا بعده
ابن ماجه 1/480 وأحمد 2/368
[Ewe Mwenyezi Mungu, msamehe aliyehai katika sisi na aliyekufa, na aliyopo na asiyekuwepo, na mdogo kati yetu na mkubwa, na mwanamume kati yetu na mwanamke. Ewe Mwenyezi Mungu unaemueka hai kati yetu basi mweke katika Uislamu, na uliyemfisha basi mfishe juu ya iman. Ewe Mwenyezi Mungu usitunyime thawabu zake wala usitupoteze baada yake.] [Imepokewa na Ibnu Maajah na Ahmad.]
اللهم إن فلان بن فلان في ذمتك،وحبل جوارك،فقه من فتنة القبر وعذاب النار،وأنت أهل الوفاء والحق .فاغفر له وارحمهُ إنك أنت الغفور الرحيم
أخرجه ابن ماجه
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika (fulani bin fulani) yuko katika dhima yako na kamba ya ujirani wako, basi mkinge na fitina ya kaburi na dhabu ya moto nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli, basi msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu.] [Imepokea na Ibnu Maajah.]
اللهم عبدك وابن عبدك وابن أمتك احتاج إلى رحمتك ،وأنت غني عن عذابه،إن كان مُحسناً فزده في حسناته، وإن كان مُسيئاً فتجاوز عنه
أخرجه الحاكم وصححه ووافقه الذهبي
[Ewe Mwenyezi Mungu, mja wako na mtoto wa kijakazi chako, nimuhitaji wa rehema yako, nawe huhitaji na kumuadhibu, kwa hivyo akiwa ni mwema mzidishie katika mema yake na akiwa ni muovu msamehe madhambi yake.] [Imepokewa na Al-Haakim na akasahihisha na kuafikiwa na Al-Dhahabiy.]
DUA YA KUMUOMBEA MAITI WAKATI ANAPOSWALIWA
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.