KINGA YA MUISLAMU
أعوذ بالله من الشيطان الرجيم واتفل على يسارك ] ثلاثاً]
مسلم 4/1729
[Najilinda na Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyelaaniwa]
Kisha utatema vijimate vichache upande wa kushoto mara tatu.
Imepokelewa kutoka kwa Uthman Ibn Al-Ass Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: [Nilimwambia Mtume ﷺ Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika shetani amenikalia kati yangu na kati ya swala yangu na kisomo changu, ananitatiza. Akasema Mtume ﷺ [Huyo ni shetani aitwae “Khanzab” ukimuhisi amekujia basi muombe hifadhi Mwenyezi Mungu nae, na tema vijimate vichache kushotoni kwako mara tatu]
……nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu akaniondoshea. [Imepokewa na Muslim.]
DUA YA ALIYEINGIWA NA WASIWASI
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.