KINGA YA MUISLAMU
[ اللهم اكفني بحلالك عن حرامك ، وأغنني بفضلك عمن سواك ]
الترمذي 5/560
[Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze mimi na halali yako kutokana na haramu, na unitosheleze kwa fadhila zako nisiwahitaji wengine usio Wewe.] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]
[ اللهم إني أعوذ بك من الهم والحزن ، والعجز والكسل ،والبخل والجبن وضلع الدين وغلبة الرجال ]
البخاري7/ 158
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na hamu na huzuni na kutoweza na uvivu na ubakhili na uoga na uzito wa deni na kushindwa na watu.] [Imepokewa na Bukhari.]
SIKILIZA DUA YA KULIPA DENI
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.