KITAAB AT-TAWHIID
باب (13) من الشرك أن يستغيث بغير الله أو يدعو غيره
وقول الله تعالى: {وَلا تَدْعُ مِنْ دُونِ اللَّهِ مَا لا يَنْفَعُكَ وَلا يَضُرُّكَ فَإِنْ فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذاً مِنَ الظَّالِمِينَ وَإِنْ يَمْسَسْكَ اللَّهُ بِضُرٍّ فَلا كَاشِفَ لَهُ إِلاَّ هُوَ وَإِنْ يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلا رَادَّ لِفَضْلِهِ يُصِيبُ بِهِ مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ} يونس:106-107
وقوله: {إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ لا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقاً فَابْتَغُوا عِنْدَ اللَّهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ وَاشْكُرُوا لَهُ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ} العنكبوت:17
وقوله: {وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنْ يَدْعُو مِنْ دُونِ اللَّهِ مَنْ لا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَنْ دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ} الأحقاف:5-6
وقوله: {أَمَّنْ يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ أَإِلَهٌ مَعَ اللَّهِ} النمل:62
وروى الطبراني بإسناده "أنه كان في زمن النبي صلى الله عليه وسلم منافق يؤذي المؤمنين، فقال بعضهم: قوموا بنا نستغيث برسول الله صلى الله عليه وسلم من هذا المنافق، فقال النبي صلى الله عليه وسلم: "إنه لا يستغاث بي، وإنما يستغاث بالله"
:فيه مسائل
الأولي: أن عطف الدعاء على الاستغاثة من عطف العام على الخاص
{الثانية: تفسير قوله: {وَلا تَدْعُ مِنْ دُونِ اللَّهِ مَا لا يَنْفَعُكَ وَلا يَضُرُّكَ
الثالثة: أن هذا هو الشرك الأكبر
الرابعة: أن أصلح الناس لو يفعله إرضاء لغيره صار من الظالمين
الخامسة: تفسير الآية التي بعدها
السادسة: كون ذلك لا ينفع في الدنيا، مع كونه كفرا
السابعة: تفسير الآية الثالثة
الثامنة: أن طلب الرزق لا ينبغي إلا من الله، كما أن الجنة لا تطلب إلا منه
التاسعة: تفسير الآية الرابعة
العاشرة: أنه لا أضل ممن دعا غير الله
الحادية عشرة: أنه غافل عن دعاء الداعي، لا يدري عنه
الثانية عشرة: أن تلك الدعوة سبب لبغض المدعو للداعي، وعداوته له
الثالثة عشرة: تسمية تلك الدعوة عبادة للمدعو
الرابعة عشرة: كفر المدعو بتلك العبادة
الخامسة عشرة: هي سبب كونه أضل الناس
السادسة عشرة: تفسير الآية الخامسة
السابعة عشرة: الأمر العجيب، وهو إقرار عبدة الأوثان أنه لا يجيب المضطر إلى الله، ولأجل هذا يدعونه في الشدائد مخلصين له الدين
الثامنة عشرة: حماية المصطفى صلى الله عليه وسلم حمى التوحيد، والتأدب مع الله
MLANGO WA 13 NI KATIKA USHIRIKINA KUTAKA KUOKOLEWA NA KUOMBA KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU ﷻ
Na kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Na wala usiwaombe wasio kuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru. Ukifanya hivyo basi utakuwa miongoni mwa walio dhulumu.Na Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea ila Yeye. Na akikutakia kheri, basi hapana awezaye kurudisha fadhila yake.Huifikisha kwa amtakaye katika waja wake, na Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.] [Yunus: 106-107]
Na kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Hakika nyinyi mnaabudu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, na mnazua uzushi. Hakika hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawakumilikiini riziki yoyote. Takeni riziki kwa Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na mumshukuru Yeye. Kwake Yeye ndio mtarudishwa.] [Al A'nkabut: 17]
Na kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Na nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanao waomba, badala ya Mwenyezi Mungu, ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama, na wala hawatambui maombi yao. Na ambao watu watakapo kusanywa watakuwa maadui zao, na wataikataa ibada yao.] [Al Ah'qaaf:5-6]
Na Amepokea At-Twabaraniy kwa Isnaad yake kwamba katika zama za Mtume ﷺ alikuwepo mnafiki akiwaudhi Waumini. Wakasema baadhi yao: “Simameni tutake kuokolewa na Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ dhidi ya huyu Mnafiki.” Mtume ﷺ akasema: [Hakika haipasi kutaka kuokolewa na mimi, bali inapaswa kutaka kuokolewa na Mwenyezi Mungu] [Atw-Twabaraaniy fiy Mu’jamil-Kabiyr]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1. Kuunganisha baina ya Du’a na “istighaathah’ kutaka kuokolewa ni kama kuunganisha baina ya jambo la ujumla na makhsusi.
2. Tafsiri ya Aya:[ Na wala usiwaombe wasio kuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru.].
3. Kufanya hivyo ni shirki kubwa.
4. Hata mtu mwema akifanya hivyo; yaani kumwomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kuwaridhisha wengine basi anakuwa mmojawapo katika madhalimu (washirikina).
5. Tafsiri inayofuatia baada yake (Suratu Yunus:107).
6. Kufanya Hivyo (Kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu), hakunufaishi duniani na juu ya hivyo ni kufuru.
7. Tafsiri ya Aya ya tatu ya (Suratul Al-‘Ankabuwt:17).
8. Kuomba riziki kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu haifai, kama vile mtu haifai kuomba Pepo ila kwake.
9. Tafsiri ya Aya ya nne ya (Suratul Al-Ahqaaf: 5).
10. Hakuna mpotovu zaidi kuliko yule anayemwomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
11. Anayeombwa si mwenye kumsikia muombaji, hana khabari ya lolote kati ya maombi ya muombaji.
12. Maombi hayo yatakuwa ni sababu ya chuki na uadui kati ya anayeomba na anayeombwa.
13. Kumuomba yeyote ni aina ya Ibaadah basi huwa ni kumwabudu unayemuomba.
14. Anayeombwa atakanusha kitendo hicho cha ‘ibaadah kinachoelekezwa kwake na mwombaji.
15. Ndio Maana ikawa mwombaji huyo ni mpotovu zaidi kuliko wote.
16. Tafsiri ya Aya ya tano ya Suratu (An-Naml: 62).
17. Jambo la ajabu ni kukiri kwa washirikina kwamba hakuna anayeweza kuondoa dhiki na shida isipokuwa Mwenyezi Mungu Pekee. Ndio maana wakiwa kwenye Shida wanaomuomba Mwenyezi Mungu hali ya kumtakasia yeye Dini.
18. Kuihami Mtume ﷺ mipaka ya Tawhiid na kuwa na Hishima na Mwenyezi Mungu ﷻ.
Today | 575 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.