MAANA SHAHADA YA LA ILAHA ILLA ALLAH
MAAN YAKE
Inamaanisha ya kwamba, hapa mola apasae kuabudiwa kwa haki illa Mwenyezi Mungu. Maana yake ni kwamba haifai kukipa chochote moyo wako wakati unafanya ibada isipokua Mwenyezi Mungu pekee.
NGUZO ZAKE
La ilaha illa Allah ina nguzo mbili: kukanusha kuabudiwa chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu, na nguzo ya pili ni kuthibitisha haki ya kuabudiwa Allah peke yake. [لا إله] [La ilaha], huku ndiko kukanusha kuabudiwa chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu sawa wawe malaika au mitume au majini au masanamu au wanadamu au miti au kaburi au chochote kile. Nayo [إلا الله] [Illa Allah], huku ndiko kuthibitisha haki ya kuabudiwa Allah peke yake.
Yafaa kueleweka kwamba nguzo hizi mbili lazima zipatikane pamoja, kwani kukanusha pekee hakutoshi , wala kuthibitisha pekee hakutoshi pia. Lazima akanushe pamoja na kuthibitisha.
Na hii ndio Nguzo muhimu katika ngozo za Uislamu kwani, mtu hakubaliwi Uislamu wake na hakubaliwi vitendo vyake mpaka akubali nguzo hii ya Shahada, kwa kukiri kwa moyo wake, na kutemka kwa ulimi wake yakuwa hakuna anaefaa kuabudiwa kwa haki ila Mwenynzi Mungu mmoja tu pekeyake, na kukiri kwa moyo wake na kutemka kwa ulimi wake ya kuwa Mtume Muhammad ni Mtume wa Mwenyzi Mungu Rehma na amani zimfikie yeye.
SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.