TAWHIYD AL-ASMAA´ WAS-SWIFAAT
Nayo ni kuamini na kumpwekesha Allah (Subhaanahu wa Ta´ala)kwa yale majina amejiita nayo nafsi yake au mtume wake amemwita nayo,na kwa zile sifa amejisifu nazo nafsi yake au mtume wake amemsifu bila ya "taatwiil" (تعطيل)(kuyakanusha majina haya au sifa hizi kwamba si zake Mwenyezi Mungu) wala "tahriif" (تحريف) (kubadilisha maana yake na kuyatoa mahala pake) wala "tak-yiif"(تكييف)(kujaribu kusema uhakiwa wa maumbile na sifa zake Mwenyezi Mungu kwamba ni hivi na hivi)na wala "tamthiil" (تمثيل)(kumfanyia mifano kwa kusema Yeye ni kama mfano wa kitu fulani katika viumbe vyake).
Dalili ya hii aina ya tauhidi ni kauli yake Allah :
[ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ} [الشورى 11}
[Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.] [Al Shuura:11]
Itikadi ya ahli sunna wal jamaa katika tauhidi hii.
1. Kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokamana na kumfananisha na sifa za viumbe, kwani Allah (Subhaanahu wa Ta´ala) hana mfano wake kabisa kabisa, sio katika dhati yake wala sifa zake wala vitendo vyake. Amesema Allah :
[ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ} [الشورى 11}
[Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.]
[Al Shuura:11]
Aya hii ina kipengele cha kukanusha kufanana chochote na Mwenyezi Mungu. Nayo ni raddi na hoja juu ya wale wanaomfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe wake:[Hapana kitu kama mfano wake], na kipengele cha kuthibitisha na kumkiria Mwenyezi Mungu yale aliojiita au kujisifu nayo, au mtume ﷺ alimwita au kumsifu nayo ambayo nayo ni raddi na hoja juu ya wale wanaompokonya na kukanusha majina au sifa zake Mwenyezi Mungu:[ Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona].
2. Kuamini kwa yale yote aliyojiita au kujisifu nayo Allah au mtume mtume ﷺ alimwita au kumsifu nayo kihakika na wala si kimajazi kama apasavyo kusifika Allah kwa kutomfananisha na yeyote au chochote katika viumbe wake wala haijuzu pia kukanusha jina au sifa yoyote aliyojiita au kujisifu nayo au mtume ﷺ amemwita au amemsifu nayo.
3. Kukata tama ya kujua uhakika wa haya majina au sifa zake Mwenyezi Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu hajatuambia uhakika wake.(1)
SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB
(1) Chanzo: Tauhidi. Daktari Hajj Makokha Maulid
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.