VIGAWANYO VYA TAWHIDI
Tawhidi inagawanyika sehemu Tutu:
1. Tawhid Al-Arrububiyah:
Ni Tawhidi ya vitendo vya Mwenyezi Mungu (S.W) nayo ni kuitakidi ya kuwa Mwenyezi Mungu (S.W) ndie muumbaji na muendeshaji wa mambo ya viumbe vyake.
Mwenyezi Mungu Anasema :
اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْفُلْكَ لِتَجْرِيَ فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْأَنْهَارَ
[Mwenyezi Mungu ndie alie umba mbingu na ardhi na ameteremsha kutoka mawinguni maji akatoa kwa maji hayo mazao hali ya kuwa ni riziki kwenu nyinyi, na akawadhalilishia majahazi ili yapite kwenye bahari kwa amri yake na akawadhalilishia nyinyi mito] [ Al-Ibrahim: 32]
2. Tawhid AL-Uluhiyyah:
Ni tawhidi ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada,nayo ni Kuitakidi ya kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndie anae stahiki kuabudiwa, wala hafai kushirikishwa na yoyote.
Mwenyezi Mungu (S.W.) Anasema :
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ} الفاتحة:5}
[Ni wewe tu tunakuabudu, na kwako wewe peke yako, tunataka msada] [Al-Fatiha: 5]
3. Tawhid Al-Asmai was-Swifaat
Ni Tawhidi ya Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake,na sifa zake,nayo ni kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu (S.W) Yuko na majina Matukufu na Sifa zake, hafanani na yoyote katika sifa zake,wala majina yake.
Na kumthibitishia Mwenyezi Mungu Sifa na Majina yote yalio kuja katika Qur'ani tukufu, na Sunna za Bwana Mtume ﷺ, bila ya kumfananisha wala kuyabadilisha.
Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ * اللَّهُ الصَّمَدُ * لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ * وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ } الإخلاص1-4}
[Sema Mwenyezi Mungu ni mmoja,Mwenyezi Mungu ndie Anaetakwa Msaada,hakuzaa wala hakuzaliwa, na hana mfano wake yoyote] [ Al-Ikhlaas: 1-4]
Na Neno lake Mwenyezi Mungu :
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ} الشورى:11}
[Hakuna chochote mfano wake,Naye ni mwenye kusikia mwenye kuona] [Al-Shuraa: 11]
Na viganyo hivi vimepatikana baada ya kuzisoma Quran na sunna zake mtume ﷺ kijumla
Amesema sheikh Mohammad Amin Ash-anqitwiy- rehema za Allah ziwe juu yake -,"Imeonyesha jumla ya Qurani tukufu kuwa tauhidi inagawanyika aina tatu: ya kwanza: tauhidurububiyya, na hii aina wameumbwa viumbe katika umbile lao la asili kuijua. Na ya pili: tauhidi ya Allah katika ibada zake, nayo ni kuhakikisha maana ya La ilaha illa Allah ambayo ina sehemu ya kukanusha na sehemu ya kukubali (kuthibitisha) . Na ya tatu: tauhidi katika majina yake Allah na sifa zake. [Adhwaa'i Al-Bayaan 3/410-411]
Na aina hizi za tauhidi zimejumulika katika kauli yake Allah:
رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا} مريم:65}
[Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi mwabudu Yeye tu, na usubiri katika ibada Yake. Je, mnamjua mwenye jina kama lake?] [Maryam 65.]
Amesema sheikh Utheimiin katika hii aya:
[Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake.]. "Hii ni tauhidurububiyyah. Na kauli Yake: [Basi mwabudu Yeye tu, na usubiri katika ibada Yake.]. Hii ni tauhidululuhiyyah. Na kauli Yake[Je, mnamjua mwenye jina kama lake?].Hii ni tauhidul-asmaa waswifaat. Yani, hammujui mwenye jina kama lake, yani, mwenye jina kama lake (somo yake)mwenye kufanana naye Allah aliyetukuka
[Al-Jawabul- Mufiid fi bayan Aqsaam Al-Twahid uk 9]
SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.