MAANA YA TAWHIDI NA UMUHIMU WAKE
Ni nini Maana ya Tawhidi:
Tawhidi ni kumpwekesha Menyezi Mungu katika Ibaada, Kumuabudu yeye peke yake, bila ya Kumshirikisha na kitu Chochote.
Na hili ndilo lengo alilo Umbiwa Mwanadamu katika huu ulimwengu kumuabudu Mwenyezi mungu na kumtii yeye peke yake.
Menyezi Mungu Anasema :
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ} الذريات:56}
[Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi] [Al-Dhariyaat:56]
UMUHIMU WA TAWHIDI
Tawhidi ni jambo bora sana,na kwa sababu hii Mwenyezu Mungu (SW) Ameshuhudia kwa nafsi yake na vile vile Malika Wameshudia,na pia walio pewa Ilimu,kuwa ALLA (S.W) ni moja na die anaefaa Kuabudiwa peke yake bila ya kushirikiswa na kitu Chochote.
Mwenyezi Mungu Anasema:
شَهِدَ اللَّهُ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ} آل عمران:18}
[Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima] [Al-Imraan:18
1. Miongoni mwa Umuhimu wa Tawhidi ni kuwa Manabii wote walikuja kulingani Watu wao Tawhidi Kumpwekesha Mwenyezi Mungu S.W Mwenyezi Mungu Anasema:
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ} النحل:36}
[Na bila ya shaka tulimpeleka mtume katika kila ummah ya kwamba : Muabuduni Mwenyezi Mungu na muapukeni muovu (Shetwani) ] [ An-Nahl: 36]
2. Mtume ﷺ: Alipo kuwa akituma Maswahaba kwenda Kulingania sehemu Fulani kwanza alikuwa akiwausia kulingania watu katika Tawhidi yaani Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (S.A) .
3.Mwenye kushikamana na Tawhidi husamehewa madhambi yake,na huepushwa na kukaa Motoni milele ,kinyume na Mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu,hatopata Msamaha wa Mola wake, Mwenyezi Mungu Anasema:
إِنَّ اللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ} النساء:48}
[Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa na husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakae ] [Al-nnisaa: 48]
4.Mwenye kushikamana na Tawhidi huwa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu,na pia hupata amani kamili na uongofu hapa Duniani na kesho Akhera.
الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ} الأنعام:82}
[Wale ambao wameamini na hawakuchanganya imani zao na dhulma watapata amani na wataongoka ] [ Al-an'aam : 82]
SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.