AL-USWUL ATH-THALATHA (Misingi Mitatu)
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمًنِ الرَّحيم
:اعْلمْ رَحِمَكَ اللهُ أَنَّهُ يَجِبُ عَلَيْنَا تَعَلُّمُ أَرْبَع مَسَائِلَ
المسألة الأُولَى: الْعِلْمُ
وَهُوَ مَعْرِفَةُ اللهِ، وَمَعْرِفَةُ نَبِيِّهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) وَمَعْرِفَةُ دِينِ الإِسْلامِ بالأَدِلَّةِ
المسألة الثَّانِيَة :الْعَمَلُ بِهِ
المسألة الثَّالِثَةُ :الدَّعْوَةُ إِلَيْهِ
المسألة الرَّابِعَةُ :الصَّبْرُ عَلَى الأَذَى فِيهِ
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
{وَالْعَصْرِ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ}
قَالَ الشَّافِعيُّ (رَحِمَهُ اللهُ): لَوْ مَا أَنْزَلَ اللهُ حُجَّةً عَلَى خَلْقِهِ إِلا هَذِهِ السُّورَةَ لَكَفَتْهُمْ
وَقَالَ البُخَارِيُّ رَحِمَهُ اللهُ: بَابُ: العِلْمُ قَبْلَ القَوْلِ وَالْعَمَلِ
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى
{فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ}
فَبَدَأَ بِالْعِلْمِ قَبْلَ القَوْلِ وَالعَمَلِ
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
Jua, Mwenyezi Mungu Akurehemu, kwamba ni wajibu wetu kujua mas-alah manne:
Suala la kwanza: Elimu:
Nayo ni elimu ya kumjua Mwenyezi Mungu, na kumjua Mtume Wake ﷺ na elimu ya kuijua Dini ya Kiislamu kwa dalili zake.
Suala la pili: Kuifanyia kazi.
Suala la tatu: Kuilingania.
Suala la nne: Kuwa na subira katika maudhi yatakayopatikana ndani yake.
Na dalili ni neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ :
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
[Naapa kwa Zama!Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara,Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri.]
Amesema Imaam Ash-Shaafi'iy (Mungu amrahamu): "Lau kama Mwenyezi Mungu Asingeliteremsha hoja kwa viumbe Vyake isipokuwa Suwrah hii, basi ingeliwatosheleza."
Na Al-Bukhari (Mungu amrahamu) amesema katika Baabul-’Ilm qablal-qawli wal-‘amal "Mlango wa elimu kabla ya kauli na ‘amali".
Na dalili ni kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako] [Muhammad:19]
Akaanza kwa elimu kwanza kabla ya kauli na ‘amali.
SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SHADDAD ALI
Today | 454 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.