Menu

 

HISTORIA FUPI KUHUSU USHIA

 

Mwanzo wa ushia unafanana na mwanzo wa kiristo wa leo,namna alivyo fanya rabbi wa kiyahudi,saul amabe alikuwa na uhasama na ukiristo,na akadai kuwa amekuwa mkiristo na akadai kuwa aliona mwanga mtakatifu na alisikia sauti ya Issa (a.s.) na kumfaya awe nabii baada yake,alibadili jina lake na kujiita Paulo.
Lengo lake hasa Lilikuwa ni kuangamiza Ukiristo na Mafunzo ya Nabii Issa (a.s.) kutoka ndani.Alikuwa mtu mwerevu na aliona njia rahisi ya kuwapotosha Wakiristo ni kukitukuza Cheo cha Nabii Issa (A.S.) kuvuka Mipaka na kuanza kumwita Mwana wa Mungu,Mshirika wa Mungu,na Kutangaza kuwa Sababu ya kusulubiwa Issa (a.s.) ni kwa Ajili ya kuwaokowa wafuasi wote wa Nabii Issa (A.S) ulimwenguni.
Haikupita karne baada ya Nabii Issa (a.s.) aliweza kuathiri Wakiristo na kuweza kubadilisha Imani ya wafuasi wa nabii issa kutoka kwenye Tawhidi (kumpwekesha mungu) na kuwapeleka katika Ushirikina,na itikadi ya utatu. Na hivyo kuweza kuabdilisha mafunzo ya Nabii Issa (A.S.) kwa wafusi wengi ila wale wachache walio kataa Unabii wa Paulo na kutahadharisha wafuasi wao.
Njama hii walio tumia Mayahudi katika Ukiristo na kuweza kufaulu ndio njia pia walio ifuata katika kubadilisha Uislamu, na kusilimu kwa lengo lakutaka kuubomoa kutoka ndani, lakini kwa kuwa allah ndie alie ahidi kunusuru Uislmu na kuuhifadhi,hawakuweza kufaulu kama walivyo weza kufaulu katika Ukirsto.
Na wakati wa zama za sayyinda Uthman (R.A) alisimu myahudi abdillah bin saba kwa lengo la kuubomoa uislamu kutokea kwa ndani ,kama alivyo fanya Paulo katika ukiristo.
Na alianza kuonyesha Unyenyekevu maalum kwa Sayyidna Ali (R.A.) kwa misingi ya undugu wake wakaribu na mtume Muhammad  na alimuhusisha na miujiza ya ajabu,na kumtukuza zaidi ya maswahaba wengine wote,na kudai kuwa alistahiki Ukhalifa baada ya Mtume ni Sayyidna ali R.a. kwa kuwa yeye ni mrithi wa Mtume  na kuanzisha shaka juu ya uaminifu na uwadilifu wa maswahaba wa mtume S.A.W. Na kutilia shaka uhalali wa Qur'ani tukufu na kuwa maswahaba R.A.Walizidisha na kupunguza,na kueneza chuki na fitna baina ya waisalmu
Na aliweza kupata lengo lake,wakati watu wa mji wa masri na miji mengine walikuwa na malalamiko dhidi ya watwala wa sayyidna Uthman (R.A) hali hii ilitumiwa vizuri na Abdillah Ibn saba katika kueneza fitna na kuwa sayyidna uthman hafai kutawala,na aliweza kushawishi watu na kupata wafuasi juu hili,na kuandaa jeshi na kulipeleka Madina kwa lengo la kumuondosha sayyidna uthma R.a.
Na walipo fika madina na Kuizunguka nyumba ya sayyidna Uthman R.A na kumtaka Ajiuzulu,sayyidna Uthman R.A. alikataa hilo,na Akawakumbusha kuwa wanavyo fanya ni kinyume na uishalmu lakini hawakumsikiliza,na walipo taka baadhi ya Maswahaba kumtetea khalifa wao na kutaka kupambana na Waasi hao, Sayyidna Uthman R.A. alikataa kumwagwa Damu ya Muislamu kwa sababu yake,na Akakhitari kufa Shaheed kuliko kusababisha umwagigaji wa Damu kwa Ummah.
Katika mazingara haya alichaguliwa sayyidna ali R.A. Kuwa khalifa wan ne kwa kuwa alikuwa chaguo stahiki.
Hata hivyo kutokana na kufa Shahidi Sayyidna Utmani (R.A.) Ummah uligawanyika makundi mawili na kutokea fitna kati ya Maswhaba na kutokea yalio tokea katika vita vya Saffin na JAMAL, Kundi la Abdillahi bin saba lilikuwa upande wa Sayyidna Ali (R.A.) na Ibn saba alinufaika kwa fitna hii ilio tokea na kuweza kupata lengo lake la kueneza fitna na chuki kati ya makundi mawili.
Na alinufaika na ujinga miongoni mwa wafuasi wake,kwa kuamini sifa bandia juu ya Sayyidna Ali (R.A) baadhi walikuja kuamini kuwa Sayyidna Ali (R.A.) Anaushirka Mungu,na kuwa Utume ulikuwa ni wa Sayyidna Ali (R.A) Lakini jibril (a.s) alifanya makosa na kumpa wahyi Bwana Mtume Muhammad .
Na khabari kama hizi zilipo mfikia siyyidna ali (R.A) alikasirika sana na kuamuwa kuwachoma moto,na katika walio chomwa ni Ibn saba .
Lakini fitna yake haikuishia hapo,bali wafuasi wake waliendeleza kazi yake Mbovu,na yaliibuka Madhehebu kwa sababu ya fitna kama hii.
Kuna wale walio utakatifu wa sayyinda ali (R.A) na kuwa wale walio dai kuwa alikuwa anastahiki kuwa mjumbe wa mungu,na wengine waliona kuwa alikuwa Mrithi wa Mtume na kuwa maswahaba walimdhulmu,na kuwa ukhalifa wa sayyidna Abubaka na umar na Uthman hakuwa wa halali,bali na kufika kuwakufurisha na kuwaita madhalimu.
Muda ulivyopita Mashia kwa mujibu wa Imani zao mbali mabli,waligawanyika makundi mengi na madhehebu mbali mbali,mpaka ya kazidi sabini.baadhi ya Madhehebu hayo hayapo tena,na badhi yako katika nchi mbali mbali lakini Madhebu yanao ongoza sasa kati ya hayo ni madhebu ya Imamia Ithna Asharia nalo ndilo dhehebu ya Jamhuri ya Irani.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6488817
TodayToday1923
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 14

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676f4d1628a7e17158665071735347478
title_676f4d1628b9015277364441735347478
title_676f4d1628ca719523445681735347478

NISHATI ZA OFISI

title_676f4d162a68b17061675531735347478
title_676f4d162a75c20344907191735347478
title_676f4d162a85218494770471735347478 Add content here

HUDUMA MPYA

: 1 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com