ITIKADI YA MASHIA JUU YA UIMAMU
Miongoni mwa itikadi za Mashia ni kuamini Maimamu kumi na mbili, na hili la uimamu ni moja katika nguzo za Uislamu kama wanavyo dai Mashia, na kuwa mtu uislamu wake haukubaliki mpaka aamini maimamu kumi na mbili,na kuwa amali ya mtu haikubaliwi mpaka awe ni mwenye kuamini maimu hawa. Kama yalivyo kuja kwenye Vitabu vyao vya kutegemewa,
Na wamemsingizia Jafar Swadi Mungu amrahamu maneno haya:
إن أول ما يُسأل عنه العبد إذا وقف بين يدي الله ـ جل جلاله ـ عن الصلوات المفروضات، وعن الزكاة المفروضة، وعن الصيام المفروض، وعن الحجّ المفروض، وعن ولايتنا أهل البيت، فإن أقرّ بولايتنا ثمّ مات عليها قُبلت منه صلاته وصومه وزكاته وحجه، وإن لم يقر بولايتنا بين يدي جل جلاله لم يقبل الله منه شيئا من أعماله
[Hakika jambo la kwanza atakalo ulizwa mja anaposimama mbele ya mola wake mtukufu ataulizwa kuhusu Swala alizofaradhiwa, na ataulizwa kuhusu zaka alizofaradhiwa, na Saumu aliyofaradhiwa na hija aliyofaradhiwa, na ataulizwa kuhusu utawala wa ahlul Bayt, ikiwa ni mwenye kuukubali utawala wetu kisha akawa ni mwenye kufa basi atakubaliwa Swala yake na funga yake na zaka zake na hija yake, na ikiwa hakukubali utawala wetu mbele ya mola alaiyetukuka hatakubaliwa chochote katika matendo yake.] [Aamali Swaduuq: uk 154]
Na wanaitakidi kuwa asiye waamini maimamu kumi na mbili basi huyo si Muislamu bali ni kafiri na ataingia motoni na akae milele humo.
Ameeleza mwanachuoni wao Al Mufiid yakuwa:
إجماع الشيعة الإمامية الاثني عشرية علَى أن من أنكر إمامة أحد من الأئمة وجحد ما أوجبه الله تعالى له من فرض الطاعة فهو كافر ضال مستحق للخلود في النار. (بحار الأنوار 8/ 366، 23/ 390، أوائل المقالات ص44).
[Wameafikiana kwa ujumla wanachuoni wa kishia wanao amini maimamu kumi na mbili yakuwa yoyote yule atakae mkanusha imamu mmoja katika katika maimamu na akapinga aliyowajibishwa na Mwenyezi Mungu mtukufu katika kumtii basi mtu huyo ni kafiri mpotevu anaestahiki kukaa motoni milele] [Biharul Anwaar 8/366,23/390 na kitabu Awaail Al Maqaalat uk 44 ]
Na wanaitakidi kuwa Maimamu wao ni Maasumin wamehifadhiwa na Madhambi kama vile Manabii na wanaitakidi kuwa wanajua ilmul Ghayb mambo yalifichika, na kuwa maimamu wao wanajua siku ya kufa kwao na wao ni bora kuliko manabii wote isipokuwa Mtume Muhammad
Kama yalivyo kuja katika kitabu chao wanachokitegemea sana
Al-Kulayniy katika kitabu ‘Uswuwlul-Kaafiy’: "Kasema Imamu Ja’afar AswSwaadiq:
[Sisi ni hazina ya elimu ya Allaah, sisi ni wafasiri wa amri za Allaah,
Sisi ni watu tuliokingwa na dhambi, imeamrishwa tutiiwe, na imekatazwa
tusiasiwe, Sisi ndio hoja ya Allaah ya wazi kwa viumbe vilivyo chini ya ardhi
na mbingu na vilivyo juu ya Ardhi.] [Usuul-ul-Kaafiy cha Al-Kulayniyiy 1/165.]
Itikadi hii ya Mashia juu ya Uimamu ni itakadi potofu kwani yaenda kinyume na Mafunzo ya Qur'ani na Hadithi sahihi za Bwana Mtume ﷺ:
zime kuja aya aya nyingi za kuthibitisha kuwa hakuna ajue Elimu ya Ghayb idipokuwa yeye Mwenyezi Mungu mtukufu Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'ani tukufu:
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّهُ} النمل:65}
[Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu.] [Al Naml:65].
Na lakustajabisha ni nguzo hii muhimu kama waanvyo dai Mashia ya kuwa amali za mja hazikubaliwi asipo amini itikadi hii ya Uimamu, kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu asitaje kwenye Qur'ani tukufu wala kushiria kama vile ilivyo kuja Swala, na zaka, na hijja, na Saumu. zimekuja aya zaidi ya moja juu yanguzo hizi tano za Uislamu, lakini hakuna aya hata moja inayoashiria itikadi hii batili Mashia.
ITIKADI YA MASHIA JUU YA MASWAHABA
ITIKADI YA MUISLAMU JUU YA MASWAHABA
Kabla ya kuelezea itakadi ya mashia juu ya Maswahaba kwanza tueleze itikadi ya Muislamu anavyo itakidi juu ya maswahaba wa Bwana Mtume ﷺ.
Sisi waislamu tunaamini kuwa Maswahaba wote ni waadilifu,na wao ndio wanafunzi bora wa Bwana Mtume ﷺ waliitetea dini hii kwa hali na mali, na walijitoa muhanga katika kuineza dini hii ya usilamu Ulimwengu mzima mpaka ukatufikia sisi.Na wao ndio waliokuwa mstari wa mbele katika mambo yote ya kheri.
Mwenyezi Mungu amewachuguwa wawe ndio wenye kusuhubiana na Mtume wake na wawe ni wenye kuisimamia Dini baada ya kufa kwake. Mwenyezi Mungu ametaja sifa zao katika Qur'ani tukufu pale alipo sema:
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا الفتح:29
[Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.] [Al Fathi:29]
Na Mwenyezi Mungu amewawelea Radhi, na alowelewa radhi na mungu hawi mbaya Maisha yote.Mwenyezi Mungu anasema:
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ التوبة:100
[Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.] [Al Tawba:100]
Na Mwenyezi Mungu ataja sifa za waumini ni kuwa wanawaombea msamaha walio watangulia kabla yao,asema Mwenyezi Mungu mtukfu:
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ} الحشر:10}
[Na walio kuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu.] [Al Hashri:10]
hii ndio itakidi ya Muislmu juu ya Maswahaba wa bwana mtume na wanaimani kuwa wao ndio watu bora katika Umma huu.
MASHIA WANAITIKIDI VIPI ?
Imejengeka itikadi ya Raafidwah juu ya kuwatukana na kuwakufurisha Maswahaba wa Mtume ﷺ Rahma na amani zishuke juu yao.
روى الكليني عن أبي جعفر رحمه الله تعالى قوله : "كان الناس أهل ردة بعد النبي صلى الله عليه وآله وسلم إلا ثلاثة . فقلت : من الثلاثة ؟ فقال : المقداد ابن الأسود ، وأبو ذر الغفاري ، وسلمان الفارسي العياشي: 1/223 الكافي: 8/245
Ametaja Al-Kulayiniy kutoka kwa Ja’afar "Waliritadi watu wote baada ya Mtume ﷺ isipokuwa watu watatu; Nikasema: Ni kina nani hao watatu? Akasema ni Miqdaad bin Aswad, na Abu Dhariy Al-Ghifaariy, na Salmaan Al-Faarisiy.]" [Al-Ayaashi 1/223] Al-Kaafiy 8/2245
عن أبي علي الخراساني عن مولى لعلي بن الحسين عليه السلام قال: كنت معه عليه السلام في بعض خلواته فقلت: إن لي عليك حقا ألا تخبرني عن هذين الرجلين: عن أبي بكر وعمر؟ فقال: كافران كافر من أحبهما
Kutoka kwa Aliy bin Al-Husayn kasema: [Nilikuwa naye (Alayhis-Salaam) katika baadhi ya sehemu alizokuwa akijitenga, nikasema kumwambia: Hakika mimi ninashakia baadhi ya haki kwako, naomba nieleze kuhusu watu hawa wawili, Abu Bakr na ´Umar, Akasema: Ni makafiri na kila mwenye kuwapenda ni kafiri.]
Pia isitoshe kuwakufurisha,bali wanawalani na kuwapiza na kuweka dua Makhsusi inayojulikana Dua ya masanamu wa kiquraish yamekuja haya katika kitabu chao ["Iqtidhaa siratul Mustaqim Mukhalafatul as'haabul jahim 1/446]
للهم العن صنمي قريش وجبتيها وطا غو تيهما وإفكيها وا بنتيهااللذين خالفا أمرك،وأنكرا وحيك،وجحدا نعامك وعصيا رسولك،وقلبا دينك، وحرفا كتابك وأحبا أعدائك وجحدا آلاءك وعطلاأحكامك .... إلى آخره
Ee Mwenyezi Mungu walaani masanamu wawili wa ki-Quraysh, na Matwaaghuti wao, na wazushi wao na mabinti wao ambao walikhalifu mamrisho yako na wakakanyusha wahyi wako na kuzikanyusha neema zako na wakamuasi Mtume wako na wakageuza Dini yako na Kugeuza kitabu chako na wakawapenda madui zako na kukanyusha ukubwa wako na kutumbiliambali hukmu zako ...
Na Dua hii mashia wameitilia umuhumu sana na wameisherehesha katika vitabu 10
imepokewa toka kwa Abu Hamzah Athumaliy kwamba alimuuliza ´Aliy bin Al-Husayn kuhusu Abu Bakr, Akasema; "Nikafiri na kila atakaemuunga mkono pia ni kafiri. [Bihaarul-Anwaar cha Al-Majlisiy 69/137-138.]
hizi ni baadi ya dondoo kwenye vitabu vyao na lau tungetaka kunukuu walio yandika kwenye vitabu vyao vyote makala yangekuwa marefu sana lakini yatosha haya tulio yanukuu,na kwa ulimwengu waleo ulimwengu wa utanda wazi yamedhihiri mengi kwa sauti na kwa Vedio za Mashekhe wao wakithibitisha itikadi hii mbya juu ya Maswaha wa Bwana Mtume ﷺ.
Msikilize huyu Sheikh wao asema wazi wazi bila yakuficha kuwa jibwa wa Ariel Sharon ni bora kuliko abuu Bakar na Omar, je kuna ukafiri zaidi ya hilo.na Baado kuna walio danganyika wakidai kuwa ni urongo wasingiziwa Mashia
ITIKADI YA AL-BADAA
Al-Badaa maana yake ni kudhihiri baada ya kutoweka, au kwa maana ya kuanzishwa kwa rai mpya. Na neno hili (Al-Badaa kwa maana zote mbili linamaanisha kuwepo hali ya kutojua jambo kisha kujua kunakuja baadae, na mambo yote haya mawili kwa Allaah ni muhali. Raafidhwah wanainasibisha sifa hii ya ( Al-Badaa) kwa Allaah.
[1/148 عن الريان بن الصلت قال: سمعت الرضا (ع) يقول:" ما بعث الله نبيّاً قط إلا بتحريم الخمر وأن يقرّ لله بالبدا" [الكليني في الكافي
Imepokewa kutoka kwa Rayyaani bin As-Swalt kwamba amesema: "Nilimsikia Ar-Ridhwaa akisema: [Hajapata Allaah kumtuma Nabii yoyote ispokuwa kwa kuharamisha pombe na kukiri (Al-Badaa) kuwa ni katika sifa za Allaah.]
Na kutoka kwa Abdullaah amesema:
["ما عبد الله بشيء مثل البداء" [أصولالكافي، كتاب التوحيد، باب البداء: 1/146
[Hajapata kuabudiwa Allaah kwa jambo lolote kama Al-Badaa.] [Usuul-Alkaafi kitabu cha Tawhidi Mlango wa Al-Badaa]
Tazama ndugu yangu Muislam jinsi wanavyomnasibishia Allaah sifa ya ujinga. Ilihali Allaah Anasema:
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّهُ} النمل:65}
[Hakuna alioko katika Mbingu na Ardhi ajuae Ghaybu (yasioonekana au yasiyojulikana) ila Allaah" [An-Naml : 65].
Badala yake wanaitakidi kuwa Maimamu wao wanajua elimu zote, wala halifichikani kwao jambo lolote. Je, hii inaweza kuwa itikadi ya Uislamu aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ́alayhi wa sallam)?
Na itikadi hii ya Al-badaa ndio itikadi ya Mayahudi kama yalivyo kuja kwenye katika cha Bibilia Mwanzo, Sura ya Sita, ya ya 5
"Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.
6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo."
CHANZO CHA ITIKADI YA AL-BADAA
Wanachuoni wakishia walikuwa wakiwaelezea wafuasi wao kuwa ungozi na utawala utarudi kwao na kuwa Dola itakuwa yao, na wakaweka mda wa miaka sabiini na kuna riwaya walio inasibisha kwa Imam Al-Jaffar Al-Swadiq juu ya hilo,ulipo pita mda huwa na kuwa yale walio kuwa wakiahidi wafuasi wao hayakutimia na wafuasi wakawa ni wenye kuliza kwa nini miaka 70 imepita na hali na Ungozi hawajarudi kwao, ndio hapo wakatafuta njia na mbinu za kutaka kuwakinaisha wafuasi wao wakanzisha itakadi hii ya Al-Badaa, Kuwa Allah subhanahu wataala ameonelea kubadilisha wakati na tarehe ya uongozi huo.
tazama haya katika kitabu cha Tafsiri Al-Ayyaashiy 2/218 na kitabu cha Al-Ghayba ukurasa 263 na kitabu cha Biharul-Anwaar 4/214
ITIKADI YA MASHIA JUU YA QUR'ANI TUKUFU
Waislamu wote duniani wanaitakidi kwamba Qur'ani ni kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu aliyetukuka kilichokamilika,Hakina shaka ndani yake na ni uongofu kwa waumini. Kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.
الم ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ} البقرة:1-2}
[Alif Lam Mim.Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu.] [Al-Baqara:1-2]
hakiingiliwi na batili mbele yake wala nyuma yake, Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema:
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ} فصلت:42}
[Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa.] [Fuss'ilat:42]
Qur-ani ni kitabu kilichopangiliwa vyema, tena kwa ufanisi na ustadi wa hali juu! Mwenyezi Mungu aliyetukuka ndiye aliyekiteremsha kitabu hiki na yeye ndiye aliyeahidi kukihifadhi.Mwenyzi Mungu anasema:
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ} الحجر:9}
[Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.] [Al-Hijr:9]
Hii ndio itikadi ya kila muislamu anavyo itakidi juu ya Qur'ani tukufu,na sasa tutizame namna wanavyo itakidi mashia juu Qur'ani tukufu, na hili ni kwa mujibu wa vitabu vyao vakutegemewa.
ITIKADI YA MASHIA JUU YA QUR'ANI TUKUFU
MASHIA wanasema kuwa hii Qur'ani tuliyonayo si Qur'an ile Aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu aliyetukuka kwa Mtume Muhammad ﷺ, bali imebadilishwa, ikazidishwa na kupunguzwa.
Wanachuoni wengi wa Shia wanaitakidi kwamba Qur'ani hii tuliyonayo ina upungufu; kwa madai ya kwamba kuna Aya zimepunguzwa hasa zile zinazotaja fadhila za Ali Ibn Abi Twalib radhi za Allah ziwe juu yake na kizazi chake, na Aya zinazompa haki ya Ukhalifa baada ya kufariki Mtume ﷺ.
Na haya ni kwa mujibu wa maneno ya Mwanachuoni wao wakutegemewa Muhammad bin Ya’aquub Al-Kulayniy, katika kitabu chake "Usuulul-Kaafiy" katika mlango aliouita, ‘Hawakuikusanya Qur-aan yote isipokuwa Maimamu’ (anakusudia Maimamu wao wa ki-Shia), kisha akaleta riwaya ifuatayo:
رواى الكليني في (الكافي) والصفار في (البصائر) عن جابر، قال: سمعت أبا جعفر (عليه السلام) يقول: "ما ادعى أحدٌ من الناس أنّه جمع القرآن كلّه كما أُنزل إلاّكذّاب، وما جمعه وحفظه كما أنزله الله تعالى إلاّ علي بن أبي طالب (عليه السلام) والاَئمّة من بعده (عليهم السلام
Kutoka kwa Jaabir, amesema: Nilimsikia Abu Ja’afar akisema: "Hajapata kudai mtu yeyote kuwa kaikusanya Qur-aan yote kama Alivyoiteremsha Allaah ispokuwa atakuwa ni muongo. Hakuna aliyeikusanya na kuihifadhi kama alivyoiteremsha Allaah isipokuwa ´Aliy bin Abi Twaalib na Maimamu baada yake." [Usuulul-Kaafi:1/228 na Al-Baswaair: 2/213.
عن جابر، عن أبي جعفر (عليه السلام)، أنّه قال: "ما يستطيع أحد أن يدّعي أنّ عنده جميع القرآن كلّه ظاهره وباطنه غير الاَوصياء
الكافي 1: 228 | 2، بصائر الدرجات: 213 | 1
Na imepokewa toka kwa Jaabir toka kwa Ja’afar kwamba amesema: "Hawezi kudai mtu yeyote kwamba anayo Qur-aan kamili isipokuwa walioachiwa wasia."
عن هشام بن سالم عن ابي عبد الله عليه السلام قال : إن القرآن الذي جاء به جبرائيل عليه السلام إلى محمد صلى الله عليه وسلم سبعة عشر ألف آية
Na imepokewa kutoka kwa Hishaam bin Saalim, toka kwa Abii Abdillaah (Ja’afar) amesema: "Hakika Qur-aan aliyokuja nayo Jibriyl kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni aayah 17,000."
Maana ya maneno hayo ni kuamanisha ya kuwa Qur'ani tuliyonayo imepungua aya nyingi sana,kwa sababu Qur'ani hii tuliyonayo iko na aya 6000 na kitu na hii ni kumanisha kuwa nusu ya mswahafu umepunguwa. Qur'ani hii ambao Mwenyezi Mungu ameahidi kuifadhi.
Anamesema mwanachuoni wa kishia katika utangulizi wa tafsiri yake naye Abul-Hasan Ibn Muhammad Twahir Al-Aamiliy,
اعلم أن الحق الذي لا محيص عنه بحسب الأخبار المتواترة الآتية وغيرها أن هذا القرآن الذي في أيدينا قد وقع فيه بعد رسول الله صلى الله عليه وسلم شيء من التغييرات ، وأسقط الذين جمعوه بعده كثيرا من الكلمات والآيات
"Jua ya kwamba, jambo la haki lisilokwepeka kutokana na habari Mutawaatiri zifuatazo na nyinginezo ni kwamba: Qur-ani hii ambayo imo mikononi mwetu imeingiliwa na mabadiliko baada ya (kufa) Mtume ﷺ Wale walioikusanya (Maswahaba) wameondosha baada ya (kufa) Mtume ﷺ
maneno mengi na Aya nyingi...."
Na mpaka kupelekea kwa Mwanachuoni wao kuandika kitabu cha kuthibtisha kuwa Qurani tulionayo imepunguwa na kubadilishwa.
HISTORIA FUPI KUHUSU USHIA
Mwanzo wa ushia unafanana na mwanzo wa kiristo wa leo,namna alivyo fanya rabbi wa kiyahudi,saul amabe alikuwa na uhasama na ukiristo,na akadai kuwa amekuwa mkiristo na akadai kuwa aliona mwanga mtakatifu na alisikia sauti ya Issa (a.s.) na kumfaya awe nabii baada yake,alibadili jina lake na kujiita Paulo.
Lengo lake hasa Lilikuwa ni kuangamiza Ukiristo na Mafunzo ya Nabii Issa (a.s.) kutoka ndani.Alikuwa mtu mwerevu na aliona njia rahisi ya kuwapotosha Wakiristo ni kukitukuza Cheo cha Nabii Issa (A.S.) kuvuka Mipaka na kuanza kumwita Mwana wa Mungu,Mshirika wa Mungu,na Kutangaza kuwa Sababu ya kusulubiwa Issa (a.s.) ni kwa Ajili ya kuwaokowa wafuasi wote wa Nabii Issa (A.S) ulimwenguni.
Haikupita karne baada ya Nabii Issa (a.s.) aliweza kuathiri Wakiristo na kuweza kubadilisha Imani ya wafuasi wa nabii issa kutoka kwenye Tawhidi (kumpwekesha mungu) na kuwapeleka katika Ushirikina,na itikadi ya utatu. Na hivyo kuweza kuabdilisha mafunzo ya Nabii Issa (A.S.) kwa wafusi wengi ila wale wachache walio kataa Unabii wa Paulo na kutahadharisha wafuasi wao.
Njama hii walio tumia Mayahudi katika Ukiristo na kuweza kufaulu ndio njia pia walio ifuata katika kubadilisha Uislamu, na kusilimu kwa lengo lakutaka kuubomoa kutoka ndani, lakini kwa kuwa allah ndie alie ahidi kunusuru Uislmu na kuuhifadhi,hawakuweza kufaulu kama walivyo weza kufaulu katika Ukirsto.
Na wakati wa zama za sayyinda Uthman (R.A) alisimu myahudi abdillah bin saba kwa lengo la kuubomoa uislamu kutokea kwa ndani ,kama alivyo fanya Paulo katika ukiristo.
Na alianza kuonyesha Unyenyekevu maalum kwa Sayyidna Ali (R.A.) kwa misingi ya undugu wake wakaribu na mtume Muhammad ﷺ na alimuhusisha na miujiza ya ajabu,na kumtukuza zaidi ya maswahaba wengine wote,na kudai kuwa alistahiki Ukhalifa baada ya Mtume ni Sayyidna ali R.a. kwa kuwa yeye ni mrithi wa Mtume ﷺ na kuanzisha shaka juu ya uaminifu na uwadilifu wa maswahaba wa mtume S.A.W. Na kutilia shaka uhalali wa Qur'ani tukufu na kuwa maswahaba R.A.Walizidisha na kupunguza,na kueneza chuki na fitna baina ya waisalmu
Na aliweza kupata lengo lake,wakati watu wa mji wa masri na miji mengine walikuwa na malalamiko dhidi ya watwala wa sayyidna Uthman (R.A) hali hii ilitumiwa vizuri na Abdillah Ibn saba katika kueneza fitna na kuwa sayyidna uthman hafai kutawala,na aliweza kushawishi watu na kupata wafuasi juu hili,na kuandaa jeshi na kulipeleka Madina kwa lengo la kumuondosha sayyidna uthma R.a.
Na walipo fika madina na Kuizunguka nyumba ya sayyidna Uthman R.A na kumtaka Ajiuzulu,sayyidna Uthman R.A. alikataa hilo,na Akawakumbusha kuwa wanavyo fanya ni kinyume na uishalmu lakini hawakumsikiliza,na walipo taka baadhi ya Maswahaba kumtetea khalifa wao na kutaka kupambana na Waasi hao, Sayyidna Uthman R.A. alikataa kumwagwa Damu ya Muislamu kwa sababu yake,na Akakhitari kufa Shaheed kuliko kusababisha umwagigaji wa Damu kwa Ummah.
Katika mazingara haya alichaguliwa sayyidna ali R.A. Kuwa khalifa wan ne kwa kuwa alikuwa chaguo stahiki.
Hata hivyo kutokana na kufa Shahidi Sayyidna Utmani (R.A.) Ummah uligawanyika makundi mawili na kutokea fitna kati ya Maswhaba na kutokea yalio tokea katika vita vya Saffin na JAMAL, Kundi la Abdillahi bin saba lilikuwa upande wa Sayyidna Ali (R.A.) na Ibn saba alinufaika kwa fitna hii ilio tokea na kuweza kupata lengo lake la kueneza fitna na chuki kati ya makundi mawili.
Na alinufaika na ujinga miongoni mwa wafuasi wake,kwa kuamini sifa bandia juu ya Sayyidna Ali (R.A) baadhi walikuja kuamini kuwa Sayyidna Ali (R.A.) Anaushirka Mungu,na kuwa Utume ulikuwa ni wa Sayyidna Ali (R.A) Lakini jibril (a.s) alifanya makosa na kumpa wahyi Bwana Mtume Muhammad ﷺ.
Na khabari kama hizi zilipo mfikia siyyidna ali (R.A) alikasirika sana na kuamuwa kuwachoma moto,na katika walio chomwa ni Ibn saba .
Lakini fitna yake haikuishia hapo,bali wafuasi wake waliendeleza kazi yake Mbovu,na yaliibuka Madhehebu kwa sababu ya fitna kama hii.
Kuna wale walio utakatifu wa sayyinda ali (R.A) na kuwa wale walio dai kuwa alikuwa anastahiki kuwa mjumbe wa mungu,na wengine waliona kuwa alikuwa Mrithi wa Mtume ﷺ na kuwa maswahaba walimdhulmu,na kuwa ukhalifa wa sayyidna Abubaka na umar na Uthman hakuwa wa halali,bali na kufika kuwakufurisha na kuwaita madhalimu.
Muda ulivyopita Mashia kwa mujibu wa Imani zao mbali mabli,waligawanyika makundi mengi na madhehebu mbali mbali,mpaka ya kazidi sabini.baadhi ya Madhehebu hayo hayapo tena,na badhi yako katika nchi mbali mbali lakini Madhebu yanao ongoza sasa kati ya hayo ni madhebu ya Imamia Ithna Asharia nalo ndilo dhehebu ya Jamhuri ya Irani.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.