SOMO LA FIQHI YA KUAMILIANA
Mlango wa kwanza unaambatana na bei (kuuza na kununuwa) na ndani yake yamo Masuala yafuatayo:
Suala la Kwanza: Maana ya bei (kuuza na kununuwa) na hukumu yake.
A) Maana ya bei (kuuza na kununuwa):
Katika lugha ya kiarabu: neno bei (biashara) lina maana ya kuchukua kitu na kupeana kitu.
Katika Sharia: Ni ubadilishanaji wa mali hata kama ni katika dhimma, au ni ubadilishanaji wa manufaa, sharti uwe ubadilishanaji huo ni wa milele, na pasiwepo ndani yake riba au mkopo.
B) Hukmu ya bei (biashara):
Bei (biashara) imeruhusiwa katika sharia ya kiislamu kwa neno lake Mwenyezi Mungu
وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ} البقرة:275}
[Na Mwenyezi Mungu amehalalisha biashara] [Suratul Baqra, Aya:275).
Na imepokelewa na Ibn Omar Mwenyezi Mungu awaele radhi, Mtume ﷺ amesema
الْبَيِّعَانِ بِالْخِيَارِ مَا لَمْ يَتَفَرَّقَا] رواه البخاري ومسلم]
[Mwenye kuuza na kununuwa, wako na Khiyari (kila mmoja wao ana uamuzi) maadamu hawajatengana] [imepokewa na Bukhari (21112) na Muslim (1531).]
Waislamu wamekubaliana juu ya kufanya biashara. Vile vile haja za watu zinalazimu kuruhusiwa kufanya biashara; kwa vile mwanadamu anahitaji anachomiliki mtu mwengine, na hakuna njia sahihi ya kupata hiyo bidhaa isipokuwa kwa kuuziana.
Juu ya hayo uislamu umeidhinisha na kuhalalisha kuuziana.
Suala la pili: Nguzo za kuuza na kununuwa.
Nguzo za kuuza na kununuwa ni tatu
1) Muuzaji na Mnunuzi
2) Bidhaa
3) Kauli kutoka kwa Muuzaji (Ijaab) na Mnunuzi (Qabul) mfano aseme Muuzaji: Nimeuza. Naye Mnunuzi aseme nimenunua. Mbali na hayo, kuna Kauli ya vitendo mfano wake; Mnunuzi apeane pesa kwa Muuzaji naye apeane bidhaa pasi na mazungumzo kati yao.
Suala la tatu: Ushahidi katika Biashara.
Inapendekeza katika uislamu kupatikane ushahidi katika kuuza na kununuwa wala si lazima, kwa mujibu wa neno lake Mwenyezi Mungu
وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ} البقرة:282}
[Na shuhudieni munapouziana] [Suratul Baqra, Aya:282].
Kutokana na aya hii, Mwenyezi Mungu ameamrisha kupatikane ushahidi wakati wakuuziana; lakini maamrisho hayo ni ya kupendekeza wala si ya kulazimishwa, kwa dalili ya aya nyingine pindi aliposema
فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ} البقرة:283}
[Na kama mmoja wenu ameweka amana na mwengine basi aliyeaminiwa airudishe amana ya mwenzake.] [Suratul Baqra, Aya:283].
Amrisho lililotokana na aya hiyo ni amrisho la uongozi; ili kupatikane uthibitisho na maslahi.
Imepokewa na Amara Bin Khuzeima, akipokea kutoka kwa babake mdogo, akisimulia khabari itokayo kwa mtume (S.A.W) kuwa “amenunua farasi kutoka kwa beduwi (mwarabu) na hakuwa na uthibitisho na hapo kuna jopo la watu walimuendea beduwi kutaka kumnunua farasi na hawakujua kuwa tayari mtume amekwisha kumnunua.”
Mafunzo yanayopatikana katika hadithi hii, lau kama ushuhuda ni jambo la lazima katika kuuzina Mtume (S.A.W) asingenunua farasi mpaka kupatikane shahidi kati yake na beduwi.
Pamoja na hayo, Maswahaba wake Mtume (s.a.w) walikuwa wakifanya biashara katika masoko bila ya uthibitisho wowote, wala haijapokewa kutoka kwao kuwa ushuhuda ni jambo la wajibu pale unapotaka kuuza au kununuwa.
Biashara hufanyika mara kwa mara katika masoko na lau ingelazimika kupatikane ushuhuda na uthibitisho baina ya watu ingepelekea kupatikana kwa mashaka kati yao.
Mbali na hayo, kama bidhaa ni yenye thamani na haikupatikana wakati huo wa kufanya biashara basi inawajibika kupatikane ushahidi; ili utumike kwa siku zifuatazo panapotokea ikhitilafu kati ya Muuzaji na Mnunuzi.
Suala la nne: Uamuzi katika biashara.
Uamuzi: Kwa kila muuzaji na mnunuzi ana haki ya kufunga mkataba wa biashara au kuvunja huo mkataba. Mbali na hayo hairuhusiwi kuvunja mkataba wa biashara ikiwa nguzo na masharti ya biashara yametimia. Lakini dini ya usilamu ni dini ya huruma, inajali matatizo na masilahi ya watu wote. Kwa ajili hii, muislamu akiuza bidhaa au akinunua kisha akajutia baada ya hapo, uislamu umemruhusu kuregelea bidhaa yake/pesa yake baada ya kuchukua uamuzi wa sawa.
Today | 739 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.