SOMO LA FIQHI
Suali: Ni nini maana ya Hisa?
Jawabu: Hisa ni sehemu anayolipwa mtu baada ya kupatikana faida katika sehemu zilizo sawa kutokana na raslimali ya mtu aliyotowa kwenye shirika la umoja wa kuchanga
Mfano wake: Shirika la umoja wakuchanga lina raslimali Dolari milioni tatu, iligawanywa raslimali yake wakati wa kufunguliwa kwake vigawanyo elfu kumi, kila kigawanyo Dolari (300), kigawanyo hichi ndio hisa, na mwenye hisa ni mshiriki katika shirika kwa kiwango cha alichonacho katika hisa.
Hukumu ya kuzunguka kwa zaka ya Hisa.
Ni Mubah, Inaruhusiwa iwapo kazi ya shirika hilo si haramu, au haina mambo yaliyoingiliana na riba.
Namna ya kutoa zaka za Hisa
Idara ya kampuni itabeba jukumu lakuwatolea zaka kwa niyaba yao ikiwa imeelezwa hilo kwenye mpango wake wa kimsingi, au awe ametegemezea hilo Yule mwenye hisa
- Idara ya kampuni ikibeba jukumu la kutoa zaka kongamano la fiqhi la umoja wa mua’tamr wa kislamu kwamba zaka zimefungamanishwa na kapuni kwa kuizingatia kuwa ni mtu wakimazangatiwa likichukuliwa kutoka kwenye kaida ya kuchanganya iliyoko kwenye sunna takatifu kuhusu zaka za wanayama, na wamezieneza baadhi ya wanavioni wa fiqihi kwa mali yote kwa kuwa huzingatiwa mali ya wote wenye kuchangia ni kama mali ya mtu mmoja na hufardhiwa zaka kwa mazingatiwa haya kuhusu kiwango na kiyasi cha zaka na mfano wa hayo
- Msimamo wa jumhuri ya wenye ilimu nikutoishika kaida ya kuchangaya katika zaka za makampuni bali huangaliwa fungu la kila mwenye kushiriki peke peke.
Na ni muhimu kutaja kwamba mkutano wapili la kongamano la kiutafiti wakiilimu umefuata maoni ya jamhuri kwenye kadhia haukushika kaida ya kuchangaya bali iliyatizama kila mali peke yake kwa hivyo ukapitisha yafuatato:
- Kwenye makampuni haya ambayo wanashiriki watu kadha hautizamwi mkusanyiko wa faida za kampuni bali huangaliwa kila yenye kumkhusu mwenye kushiriki pekeyake
- na niwajibu juu ya idara ya kampuni kuweka mbali hisa zisizopaswa na zaka kama hisa za waqfu ya mambo ya kheri, na hisa za makundi ya mambo ya kheri, na asili ya mali thabiti, ambavyo hayapaswi na zaka kama majengo, na maofisi na vyombo, na magari mahsusi na kampuni ikitowatolea zaka hapo itawalazimu wenye hisa kujitolea wenyewe kwa namna ifuatayo:
1. Hisa za makampuni za makulima hutolewa zaka zake kama zaka za nafaka na matunda.
2. Hisa za makampuni ya biashara hutolewa zaka zake, mali ya asili na faida zote, na hukisiwa hisa kwa kima cha sokoni wakati wakuwajibika zaka.
3. Hisa za makampuni ya sanaa hutolewa zaka zake faida safi wala sio vyombo vya kukodisha na majengo na mfano wake.
4. Akiuza mwenye hisa hisa zake wakati wa kupitiwa na mwaka yatakuswanya thamani ya mali yake, na atayatolea zaka, ama mwenye kunuwa atatolea hisa alizo nunuwa kwa namna ilivo tangulia.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.