Menu

SOMO LA FIQHI


  somo lafiqhi


Mapambo ya wanawake yako sampuli mbili: Mapambo ya dhahabu na fedha, na mapambo yasiyokuwa ya dhahabu wala fedha.

1. Mapambo ya dhahabu na fedha.
Kitengo cha kwanza: Mapambo yaliyokusudiwa kwa lengo la kuhifadhiwa au kuwekwa kama akiba ya baadaye kunapotokea jambo, au imenunuliwa kwa nia ya kufanya biashara, basi zaka hapa ni lazima kutoa.

Kitengo cha pili: Mapambo yaliyokusudiwa kwa lengo la kutumiwa, basi uzuri zaidi ni kuitolea zaka ili kijiepusha na lawama,kwa Hadithi hii

 

وعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ عَنْ أَبِيهِ عَنْ جَدِّهِ أَنَّ امْرَأَةً أَتَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمَعَهَا ابْنَةٌ لَهَا ، وَفِي يَدِ ابْنَتِهَا مَسَكَتَانِ غَلِيظَتَانِ مِنْ ذَهَبٍ ، فَقَالَ لَهَا : أَتُعْطِينَ زَكَاةَ هَذَا ؟
قَالَتْ : لا 
قَالَ : أَيَسُرُّكِ أَنْ يُسَوِّرَكِ اللَّهُ بِهِمَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ سِوَارَيْنِ مِنْ نَارٍ ؟
قَالَ : فَخَلَعَتْهُمَا ، فَأَلْقَتْهُمَا إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، وَقَالَتْ : هُمَا لِلَّهِ عَزَّ وَجَلَّ وَلِرَسُولِهِ      رواه أبوداود

 

Kutoka kwa Amru bin Shuayb kutoka kwa baba yake kutoka kwa Babu yake kwamba  mwanamke mmoja alimjilia Mtume ﷺ pamoja na binti yake, na mkononi mwa binti yake kuna bangili mbili nzito za dhahabu, (Mtume ﷺ) akamwambia: [ Je watolea zaka hizi bangili] Akasema: Hapana. Akasema (Mtume ﷺ): [Je utafurahia Mwenyezi Mungu akuvalishe bangili kwa hizi bangili mbili za moto?] Akasema: Yule binti akazivua, akampatia Mtume ﷺ, kisha akasema: “Hizo ni za Mwenyezi Mungu na Mtume wake”   [Imepokewa na Abu Daud.]

Na kuna wanavyuoni ambao hawawajibishi mapambo ya wanawake kutolewa zaka, kwasababu hayo mapambo sio mali inayotarajiwa kukua, lakini ni pambo la mtu binafsi yuwatumia na kunufaika nayo kama vile nguo na fanicha na vyombo, na ni katika mahitajio ya mwanamke na virembesho vyake, na asili ya mali ni kukua au kuweza kukuzwa ndio ilazimike kutolewa zaka.

Na ubora wa hali ni mtu kutoa zaka kwa mapambo yaliyokusudiwa kwa matumizi ambayo si kinyume na sheria na kwa lengo la kujirembesha; kwasababu kauli hii iko katika hali nzuri zaidi na kujiondoa kwa lawama; kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

دع ما يريبك إلى ما لا يريبك]     رواه البخاري] 

 

[Wachana na linalokutia shaka na ufanye lile lisilokutia shaka]     [Imepokewa na Bukhari].

2. Mapambo Yasiyo kuwa ya Dhahabu wala Fedha.
Kama vile almasi, yakut, lulu, na mfano wa hizi, basi vitu hivi havitolewi zaka hata vikawa vingi kiasi gani, isipokuwa vikikusudiwa kwa lengo la biashara vitatolewa zaka vitakuwa vimeingia katika mali ya biashara.


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6573248
TodayToday1315
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 24

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682883e3f29674418670691747485667
title_682883e4107759693373821747485668
title_682883e4108fc16316771761747485668

NISHATI ZA OFISI

title_682883e412e0920233402741747485668
title_682883e412f9521275223001747485668
title_682883e4130f010857871151747485668 Add content here

HUDUMA MPYA

: 7 + 3 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com