Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Suali: Ni zipi Faradhi za udhu?

Jawabu: Faradhi za Udhu ni sita
1.Kutia nia. kwa neno lake Mtume:

 

إنَّما الأَعمالُ بالنِّيَّات]    رواه البخاري]

 

[Hakika (kusihi) ibada ni kwa (kupatikana) nia]   [Imepokewa na Bukhari]

Na mahali pake ni moyoni, wala haitamkwi. Na lau mtu afanya matendo ya kutawadha kwa lengo la kujiburudisha au kujinadhifisha, bila ya nia ya kutawadha, basi hilo halimtoshelezi.

2. Kuosha uso. Na miongoni mwa huko ni kusukutua na kupaliza puani.

3. Kuosha mikono miwili pamoja na vifundo viwili.

4. Kupangusa kichwa chote, pamoja na masikio mawili

5. Kuosha miguu miwili pamoja na vifundo viwili.

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ}   المائدة:6}

 

[Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni]   [Al Maaida:6]

6. Kufuatanisha beina ya viungo.

haya yamethibitika kutokana na hii Aya iliofunza juu ya udhu - Al Maida : 6, kwani “wau” iliomo kwenye Aya hii ni yenye kueleza juu ya mpangilizio. Pia haikupokewa kuwa Mtume wetu amewahi kutawadha bila ya mpangilizio kama ulivyokuja kwenye Aya hii.

Vilevile ameeleza Mtume wetu ﷺ alisema baada ya kukamilisha kutia udhu maneno yenye maana kama hivi:

 

هَذَا وُضُوءُ مَنْ لا يَقْبَلُ اللَّهُ مِنْهُ صَلاةً إِلا بِهِ]    رواه البخاري]

 

[Huu ndio udhu, hakubali Mwenyezi Mungu Mtukufu Sala ila kwa udhu kama huu]  [Imepokewa na Bukhari]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668143
TodayToday831
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 8

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6866b548ea74e19092106141751561544
title_6866b548ea8443165494001751561544
title_6866b548ea92717226692831751561544

NISHATI ZA OFISI

title_6866b548ebeac1591196851751561544
title_6866b548ebf9d12923010291751561544
title_6866b548ec0824460619731751561544 Add content here

HUDUMA MPYA

: 15 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com