SOMO LA FIQHI
Suala: Ni yapi Masharti ya kutawadha?
Jawabu: Masharti ya kutawadha ni kama yafuatavyo
1. Maji yawe twahara.
2. Maji yawe yafaa kutumiwa, yasiwe ya kuiba, kwa mfano.
3. Kuondoa chochote chenye kuzuia maji kufika kwenye ugozi, kama vile mafuta ya mshumaa na mfano wake.
4. Kumaliza na kukatika kinacho sababisha kutawadha, kwa mfano mtu kutawadha na huku bado hajamaliza kukidhi haja yake.
5. Kukatika kwa damu ya Hedhi na Nifasi kwa Mwanamke, lau atatawadha mwanamke mwenye Hedhi au Nifasi basi Udhu wake hautasihi.
6. Kuingia kwa wakati kwa mtu mwenye Hadathi ya daima kama mwenye ugonjwa wa kutokwa na mikojo au Mwanamke mwenye damu ya Istihadha (Damu ya ugonjwa).
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.