Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


KUMTANGULIA IMAMU KATIKA SWALA

1. Amri ya Sheria ni kuwa maamuma amfuate imamu wake kwa kufanya kitendo anachofanya imamu wake papo kwa papo, kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

إِنَّمَا جُعِلَ الإِمَامُ لِيُؤْتَمَّ بِهِ، فَإِذَا كَبَّرَ فَكَبِّرُوا، وإِذَا سَجَدَ فَاسْجُدُوا]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Imamu amewekwa afuatwe: akipiga takbri, na nyinyi pigeni takbiri, na akisujudu, na nyinyi sujuduni]     [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Imeharamishwa kumtangulia imamu, na Mtume alilitilia hilo makazo mkubwa kwa kusema:

 

أما يخشى الذي يرفع رأسه قبل الإمام أن يحول الله رأسه رأس حمار]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Kwani haogopi ambae anaeinuwa kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu amgeuze kichwa chake akifanye kichwa cha punda]    [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3. Mwenye kumtangulia imamu wake kwa kusahau itamlazimu arudi amfuate.

 

TANBIHI:

Kuswali nyuma ya asiye na Twahara
Swala Haisihi nyuma ya asiye na twahara isipokuwa iwapo hakujulishwa kuwa hana udhu mpaka baada ya kumalizika Swala. Na katika hali hii inasihi swala ya maamuma, na ni juu ya imamu arudie Swala.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6785500
TodayToday501
Highest 07-17-2025 : 4917
US
Guests 24

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68a98c24b0cf42966647381755941924
title_68a98c24b0de01300998931755941924
title_68a98c24b0ec4228282541755941924

NISHATI ZA OFISI

title_68a98c24b24f94856172211755941924
title_68a98c24b25ec20744091491755941924
title_68a98c24b26b89955552381755941924 Add content here

HUDUMA MPYA

: 15 + 4 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com