Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi  


FADHILA ZA ADHANA

Zimepokelewa hadithi kadhaa kutoka kwa Mtume wa Allah zinazofahamisha fadhila na thawabu kubwa zinazopatikana ndani ya adhana.

Miongoni mwa hadithi hizo ni kama zifuatavyo:

1. Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah  radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema:

 

لو يعلم الناس ما في النداء والصف الأول ثم لم يجدوا إلا أن يستهموا عليه لاستهموا]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Lau watu wangelijua yaliyomo katika wito (adhana) na safu ya kwanza (ya swala ya jamaa) Kisha wasipate (fursa hizo) ila kwa kupiga kura, basi wangelipiga kura.] [Imepokewa na Bukhaari na Muslim]

2. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Said Al-khudriy  Radhi za Allah ziwe juu yake  amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ :

 

إني أراك تحب الغنم والبادية، فإذا كنت في غنمك وباديتك فأذنت بالصلاة، فارفع صوتك بالنداء، فإنه لا يسمع مدى صوت المؤذن جن، ولا إنس، ولا شيء، إلا شهد له يوم القيامة      رواه البخاري

 

[Mimi nakuona unapenda (kuchunga) mbuzi na kukaa Baadiya (majangwani) utakapokuwa Badia na mbuzi wako ukaadhini kwa ajili ya Swala Basi inyanyue sauti yako kwa wito huo (adhana) kwani hakika haisikii sauti ya muadhini jini wala mwanadamu wala kitu cho chote ila (sauti hiyo) itamshuhudia siku ya kiyama.]     [Imepokewa na Bukhari]

3. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amewaombe Mungu wenye kuadhini na akaomba kwa kusema: 

 

اللَّهُمَّ أَرْشِدِ الْأَئِمَّةَ، وَاغْفِرْ لِلْمُؤَذِّنِينَ]     اخرجه أبوداود وصححه الألباني]

 

[Ewe Mwenyzi Mungu waongoze maimamu na na uwasamehe wenye kuadhini]                [Imepokewa na Abuu Dawud na kusahihishwa na Al Baaniy]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668042
TodayToday730
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 13

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68669c122122619976556121751555090
title_68669c12213108441554001751555090
title_68669c12213f611807435721751555090

NISHATI ZA OFISI

title_68669c12229e915233395891751555090
title_68669c1222ac51836088421751555090
title_68669c1222b9b10634934991751555090 Add content here

HUDUMA MPYA

: 9 + 12 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com