Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


MAANA YA ADHANA

Adhana ni neno la Kiarabu lenye maana mbili; maana ya kilugha na maana ya kisheria Kilugha neno adhana lina maana ya “tangazo” kama lilivyotumika ndani ya Qur'ani Tukufu:

 

وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّهَ بَرِيءٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ}    التوبة:3}

 

[Na ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina] [Tawba:3]

Ama maana ya adhana kisheria: Ni (dhikri) utajo maalum iliyowekwa na Uislamu kwa ajili ya kutangaza kuingia kwa wakati wa swala ya fardhi na kuwaita waislamu kuja kuswali

MAANA YA IQAAMA

Ni kujulisha kuanza kuswaliwa kwa kuleta utajo (dhikiri)maneno maalumu.

HUKMU YA KUADHINI NA KUQIMU
1. Katika Swala za jamaa:
Ni faradhi ya kutosheleza, kwa Swala tano za faradhi peke yake, sawa mtu akiwa safarini au mjini, kwa kuwa hizo mbili ni miongoni mwa alama za Uislamu za waziwazi, hivyo basi haifai kuziacha. Amesema Mtume :

 

وإذا حضرت الصلاة فليؤذن لكم أحدكم، وليؤمكم أكبركم]   متفق عليه]

 

[Ufikapo Wakati wa Swala, basi awaadhinie mmoja wenu, kisha awaswalishe mkubwa wenu]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Katika Swala ya anayeswali peke yake:
Ni sunna. Amepokewa kutoka kwa Uqbah bin Amir akisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema:

 

يعجب ربكم من راعي غنم في رأس شظية بجبل يؤذن بالصلاة ويصلي فيقول الله عز وجل انظروا إلى عبدي هذا يؤذن ويقيم الصلاة يخاف مني قد غفرت لعبدي وأدخلته الجنة     رواه أبوداود والنسائي

 

[Anamuonea ajabu Mola wako mchunga mbuzi aliye juu ya kilele cha jabali, anayeadhini kwa Swala kisha akaswali, hapo aseme Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: “Mwangalieni mja wangu huyu, anaadhini kisha anakimu Swala, ananiogopa! Nishamsamehe mja wangu na nitamuingiza Peponi]     [Imepokewa na Abuu Dawud na Annasai.]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6573237
TodayToday1304
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 37

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6828805165f2c14425291671747484753
title_682880516609220070414281747484753
title_68288051661f620077692031747484753

NISHATI ZA OFISI

title_6828805172bb817862585991747484753
title_6828805172c9f19696253711747484753
title_6828805172d752060209851747484753 Add content here

HUDUMA MPYA

: 1 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com