SOMO LA FIQHI
1. Inahisabika kuwa mtu amesimama arafa kwa kuweko mwenye kuhiji uwanja wa arafa siku ya tisa, sawa akiwa amesimama ama amekaa ama amelala ama amepanda, na silazima kuwa amesimama.
2. Kusimama arafa ni Nguzo miongoni mwa nguzo za Hijja na haisihi Hija ya mtu ikiwa hakusimama Arafa, na mwenye kukosa kusiamam Arafa huwa ameikosa Hija kwa neno lake Mtume ﷺ:
الحج عرفة ] رواه احمد والترمذي]
[Hija ni Arafa] [Imepokewa na Ahmad na Attirmidhiy]
3. Unaanza wakati wa kisimamo cha Arafa kuanzia kutoka kwa Alfajiri siku ya tisa mpaka Alfajiri ya siku ya kumi, mwenye kusiama Arafa katika wakati huu japo kidogo hali yakuwa ni mtu afaaye kusimama hija yake itasihi, na mwenye kukosa kusimama wakati huu hija yake haikusihi Amepokea Ibnu Abbas kutoka kwa Mtume ﷺ Amesema:
من أدرك عرفة قبل أن يطلع الفجر فقد أدرك الحج] رواه الترمذي]
[Mwenye kuipata arafa kabla ya Alfajiri basi ameipata hija] [Imepokewa na Attirmidhiy na Amesahihsha Al’albaniy katika swahihil-jaami’ No(5995)]
4. Arafa yote ni uwanja wa kisimamo, na Mtume ﷺ alisimama kwenye jabali karibu na Swakharaat hali yakueleka kibla na wala hakupanda juu ya jabali Amesema:
ووقفت ههنا. وجمع كلها موقف] رواه مسلم]
[Nimesimama hapa na Arafa yote ni sehemu ya kisimamo] [Imepokewa na Muslim]
ikiwa ataweza kusimama alipo simama Mtume ﷺ ni uzuri na asipo weza atasimama sehemu yoyote, wala haifai kusimama kwenye jangwa wala kupanda jabali,
5. Ni juu ya mwenye kuenda hijja akumbuke kuwa siku ya Arafa ni siku kubwa na ina fadhla kubwa, na Mwenyezi Mungu anawakirimu waja wake, na ajifakhiri mbele ya malaika wake, na nisiku ambao watu huacha huru na moto.
Amesema Mtume ﷺ:
ما من يوم أكثر من أن يعتق الله فيه عبدا من النار من يوم عرفة وإنه ليدنو ثم يباهي بهم الملائكة فيقول : ما أراد هؤلاء] رواه مسلم]
[Hakuna siku ambao Mwenyezi Mungu huacha waja wake huru na moto kuliko siku ya Arafa, na siku hiyo Mwenyezi Mungu anakurubia kisha anajifakhirisha na waja wake kwa Malaika, na anasema: wataka nini wajawangu hawa?] [Imepokewa na Muslim] yatakikana kwa hajji kufaidika na masaa ya siku hii tukufu, na kujadidisha Tawba na kujihisabu nafsi yake wala asipoteze wakati wake kwa kuzunguka ovyo na kuzungumza upuzi na kufanya mijadala.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.