SOMO LA FIQHI
1. KUOGA
Khaarijah bin Zaid bin Thaabit radhi za Allah ziwe juu yake alipokea kutoka kwa baba yake kwamba alimuona Mtume ﷺ akivua nguo na kuoga kwa sababu ya kuhirimia Hija [Imepokewa na Tirmidhi.]
2. KUJISAFISHA
Nako ni kuondoa nywele za makapwa yake na kinena chake na kupunguza masharubu yake na kucha zake.kwa sababu ni katika Sunna za kimaumbile kama alivyo sema Mtume ﷺ:
خمس من الفطرة الختان والاستحداد وتقليم الأظفار ونتف الإبط وقص الشارب] رواه البخاري ومسلم]
[Mambo matano ni katika (Sunna) za kimaumbile kutahir,na kunyoa nywele sehemu za siri,na kukata kucha,na kusumua nywele za makapwa na kupunguza Masharubu]. [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
3. KUJITIA MANUKATO
Kwa hadithi iliyopokewa na Aishah radhi za Allah ziwe juu yake kwamba alisema:
كنت أطيب رسول الله صلى الله عليه وسلم لإحرامه حين يحرم] رواه البخاري ومسلم]
[Nilikuwa nikimtia manukato Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ihramu yake anapohirimia] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Wala hazitii manukato nguo zake, kwa kauli ya Mtume ﷺ:
وَلَا تَلْبَسُوا مِنَ الثِّيَابِ شَيْئًا مَسَّهُ الزَّعْفَرَانُ وَلَا الْوَرْسُ [ الورس: هو نبات أصفر طيب الريح يُصْبَغ به] متفق عليه]
[Na msivae nguo yoyote iliyopakwa zafarani wala manukato ya wars [ Alwars: nimmea wa majano wenye harufu mzuri] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
4. KUVUA NGUO ZA KUSHONA
[Makhiitw: Kila nguo iliyoshonwa kwa kipimo cha kiungo au juu ya mwili wote, mfano wa kanzu na suruali.] kabla ya kuhirimia [Ama baada ya kuhirimia, ni lazima kwake avue nguo za mzunguko, kwa kuwa hizo ni miongoni mwa vitu] na kuvaa shuka ya chini na ya juu zilizo nyeupe na viatu.
Kwa kauli yake Mtume ﷺ:
وَلْيُحْرِم أَحَدُكُمْ فِي إِزَارٍ وَرِدَاءٍ وَنَعْلَيْنِ، فَإِنْ لَمْ يَجِدْ نَعْلَيْنِ فَلْيَلْبَسْ خُفَّيْنِ، وَلْيَقْطَعْهُمَا حَتَّى يَكُونَا إِلى الْكعْبَيْ] رواه أحمد]
[Na ahirimie mmoja wenu akiwa na shuka ya chini na ya juu na viatu. Akikosa viatu, avae khofu mbili, na azikate mpaka kwenye vifundo vya mguu] [Imepokewa na Ahamad]
Ama mwanamke atavaa nguo anazo taka, wala hakuna nguo ya rangi maalumu, lakini ajiepushe na kufanana na Wanaume na nguo za mapambo, na wala havai nikabu na soksi za mikono [Quffaaz: nguo inayovaliwa na mwanamke kufinika mkono] katika kuhirimia.ila akiwa kati ya wanaume ajnabi atateremsha nguo yake na kuufunika uso wake, kwa ilivyo thubutu kutoka kwa bibi Aisha radhi za Allah ziwe juu yake Amesema
كَانَ الرُّكْبَانُ يَمُرُّونَ بِنَا وَنَحْنُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُحْرِمَاتٌ، فَإِذَا حَاذَوْا بِنَا سَدَلَتْ إِحْدَانَا جِلْبَابَهَا مِنْ رَأْسِهَا عَلَى وَجْهِهَا فَإِذَا جَاوَزُونَا كَشَفْنَاهُ رواه أبوداود
[Ulikuwa msafara unapo pita mpele yetu na sisi tukiwa na Mtume ﷺ Kwenye ihraamu wakiwa mkabala na sisi akitermsha mmoja wetu jilbabu yake akifunika uso wake wakitupita tukifunuwa] [Imepokewa na Abuu Daud.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.