SOMO LA FIQHI
Suali: Ni nini Maana ya Umra
Jawabu: Maana ya Umra Umra kilugha ni Ziara
Ama maana yake kisheria
Ni kuizuru Nyumba Takatifu (Alkaba) wakati wowote mtu anapotaka, kwa kutekeleza matendo ya ibada maalumu.
Suali: Ni ipi Hukumu ya Umra na fadhla zake
Jawabu: Umra ni wajibu wa mara moja katika umri kama vile hajji. Kwa neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّهِ} البقرة:196}
[Na timizeni Hija na 'Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu]. [Al Baqara : 196]
Na kwa kauli yake Mtume ﷺ :
الإسلام أن تشهد أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله ، وتقيم الصلاة ، وتؤتي الزكاة ، وتحج البيت وتعتمر ، وتغتسل من الجنابة ، وتتم الوضوء ، وتصوم رمضان ) رواه إبن خزيمة والدار قطني, وقال الدارقطني : هذا إسناد ثابت صحيح
[Uislamu ni ukubali kwamba hakuna mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na usimamishe Swala, na utoe Zaka, na uikusudie Alkaba kwa ibada ya Hija na ufanye Umra, na uoge kutokana na janaba, na ukamilishe udhu, na ufunge Ramadhani] [Imepokewa na Ibnu Khuzaimah na AL-Ddaar Qutiniy na akasema isnadi yake ni thaabit na nisahihi]
Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:
العمرة إلى العمرة كفارة لما بينهما والحج المبرور ليس له جزاء إلا الجنة] رواه البخاري ومسلم]
[Umra mpaka Umra ni kafara ya dhambi baina yake, na Hija iliyokubaliwa haina malipo isipokuwa Pepo] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.