Menu

SOMO LA FIQHI


  somo lafiqhi


Suali: Ni yapi masharti ya Kuwajibika Hijja ?
Jawabu: Kuwajibika Hijja kuna shuruti tano:
Ya Kwanza, kuwa ni Muislam,

kwani Hija ni ibada sawa na ibada nyengine kama vile, Sala, Saumu, Zaka. Kwa sababu kafiri ibada zake hazikubaliwi .Kwa neno lake Mwenyai mungu mtukufu:

 

وَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَاتُهُمْ إِلَّا أَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّهِ وَبِرَسُولِهِ}  التوبة:54}

 

[Na hawakuzuiliwa kukubaliwa michango yao ila kwa kuwa walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake,]    [Al Tawba:54]

Ya Pili, kuwa ni balegh,

Mtoto mdogo kabla ya balegh halazimiki na Hija; sawa na ibada nyengine. Hivi ni kwa neno lake Mtume :

 

 

رُفِعَ الْقَلَمُ عَنْ ثَلاثَةٍ : عَنْ النَّائِمِ حَتَّى يَسْتَيْقِظَ ، وَعَنْ الصَّبِيِّ حَتَّى يَحْتَلِمَ ، وَعَنْ الْمَجْنُونِ حَتَّى يَعْقِلَ]     رواه أبوداود]

 

[Imeinuliwa kalamu kwa watu watatu (hawaandikiwi dhambi) aliyelala mpaka azunduke, mtoto mapaka abaleghe na mwendawazimu mpaka apate akili]   [Imepokewa na Abuu Daud].

Lakini lau mtoto mdogo atahirimia hija basi hija yake itasihi.Hii ni kwa hadithi ya Ibnu ‹Abbas radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mwanamke mmoja alimuinulia Mtume wa Mwenyezi Mungu mtoto, na akasema: «Je, huyu ana Hija? Mtume akasema:

 

نعم ، ولك أجر]    رواه مسلم]

 

[Ndio, nawe una thawabu]    [Imepokewa na Muslim.].

Lakini haimtoshelezi na Hijja ya Uislamu, na itahesabiwa ni Sunna,na atakapo baleghe atawajibika kuhiji tena ikiwa na uwezo.

Ya Tatu, awe ni mwenye akili timam;

mgonjwa wa akili mwenda wazimu haimlazim Hija, sawa na ibada nyengine. Kwa hadithi iliyotangulia. 
Ya Nne, kuwa huru,

Asie kuwa huru hawajibikiwi na Hija, kwa sababu anakuwa ni mwenye kumtumikia bwana wake,huwajibikiwa na Hija pale anapokuwa huru. Kwa hadithi ya Mtume:

 

أيما عبد حج ثم عتق فعليه حجة أخرى]    رواه أحمد والبهقي والحاكم]

 

[Mtumwa yeyote yule akihiji kisha akapewa uhuru, itamlazim ahiji tena].   [Imepokewa na Ahmad na Al Bayhaqiy na Al Haakim].

Lakini sharti hili limeondokwa kwa kutoweko watumwa zama zetu hizi.
Ya Tano, Kuwa na uwezo.

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنْ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلا}   آل عمران:97}

 

[Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea……".]    [Al 'Imraan : 97].

Sita. Kwa Mwanamke awe na maharimu yake

[Mahram: ni yule ambaye ni haramu kwa mwanamke kuolewa naye kama baba, ndugu na mjomba.] 

Kwa hadithi ya Ibnu ‹Abbas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema: Nilimsikia Mtume akisema:

 

 

لا تُسَافِرْ الْمَرْأَةُ إِلا مَعَ ذِي مَحْرَمٍ]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Hasafiri mwanamke isipokuwa pamoja na mtu maharimu yake].  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Akainuka mtu mmoja akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mke wangu ametoka kwenda kuhiji, na mimi nimejisajili katika vita kadha na kadha. Akasema Mtume ﷺ: [Toka uende kuhiji na mkeo]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487635
TodayToday741
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 61

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e6922e24a615745035701735289122
title_676e6922e260810013594561735289122
title_676e6922e27512084357211735289122

NISHATI ZA OFISI

title_676e6922e4d0310191867951735289122
title_676e6922e4e298124622921735289122
title_676e6922e4f4d3019322421735289122 Add content here

HUDUMA MPYA

: 13 + 3 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com