Menu

HUKMU YA MWANAMKE WA KIISLAMU KUVAA WIGI KWA AJILI YA KUMPABIA MUMEWE


Suali?

Ni ipi hukmu ya mwanamke kuvaa (Mawigi) au nywele za kuvisha ili ajipambe kwa ajili ya mume wake ?
Jawabu :
Alhamdulillah , inatakiwa kwa Mume na Mke kijipamba kwa ajili ya mwenza wake kwa anacho kipenda, na atie nguvu mahusiano baina yao lakini katika mipaka yaliyohalalishwa na Sheria ya Kiislamu sio yaliyoharamishwa na sheria, na kuvaa Mawigi ilianza kuvaliwa na wanawake wasiokua Waislamu na wakajulikana kwa kuvaa mawigi na kujipamba nayo mpaka ikawa ni alama yao, hivyo basi Mwanamke kuvaa Wigi na kujipamba nayo hata kama ni kwa ajili ya Mume wake kuna kujifananisha na makafiri, na Mtume Muhammad amekataza jambo hilo kwa neno lake:

 

مَنْ تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ]    رواه أبوداود]

 

[Atakaejifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao]   imepokewa na Abuu Dawud

na kwa sababu Wigi inaingia katika hukmu ya kuunganisha nywele bali ni mbaya zaidi kuliko kuunganisha nywele na Mtume amekataza jambo hilo na akamlaani mwenye kulifanya .
Fatwa za kamati ya kudumu ya fatwa 5/191.
Na amepokea Humeid bin Abdulrahman bin Auf yakwamba yeye amemsikia Muawiya bin Abi Sufyan (Radhi za Allah ziwe juu yao) mwaka wa Hijja na yeye akiwa juu ya Mimbar na yeye anasema na akachukua fungu la nywele ambalo lilikua katika mkono wa mlinzi wake wapo wana zuoni wenu nimemsikia Mtume rehma na amani ziwe juu yake akikataza jambo kama hili na anasema : kwa hakika waliangamia wana waisraeli pale wanawake wao walipojifanyia vitu hivi (yaani nywele za Kubandika).na imepokelewa kutoka kwa Abu Hureirah radhi za ALLAH ziwe juu yake kutoka kwa Mtume Muhammad ﷺ amesema:

 

لَعَنَ اللَّهُ الْوَاصِلَةَ وَالْمُسْتَوْصِلَةَ وَالْوَاشِمَةَ وَالْمُسْتَوْشِمَةَ]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Mwenyezi Mungu amemlaani mwanamke mwenye kuunganisha nywele na mwenye kuunganishiwa na mwenye kuchora Tatoo na mwenye kuchorewa]  [imepokelewa na Bukhary na Muslim]

na ALLAH ndie mjuzi zaid


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6488846
TodayToday1952
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 21

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676f5452895198447355131735349330
title_676f5452895fe21161954181735349330
title_676f5452896e315990917231735349330

NISHATI ZA OFISI

title_676f54528accb562423121735349330
title_676f54528adab20935401291735349330
title_676f54528ae9120965912731735349330 Add content here

HUDUMA MPYA

: 10 + 7 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com