HUKMU YA KULA MATUNDA YALIOPANDWA KATIKA MAKABURI
Suali? Ni nini hukmu ya kula matunda yaliyopandwa katika makaburi ?? Na ni nini hukmu ya kunywa maji yanayochimbuka katika makaburi??
Jawabu:
Alhamdulillah baada ya kumshukuru ALLAH na kumswalia Mtume Muhammad ﷺ:
yaliyo sahihi katika maneno ya wanazuoni ni kwamba kula Matunda yaliyopandwa katika Makaburi na kunya Maji ambayo yanachimbuka katika makaburi haina tatizo, kwani waliochukia jambo hili katika wanazuoni wamechukia kwa kuhofia Matunda yale au Maji yale kuchanganyikana na Najisi.Kama vile usaha wa maiti na damu yake na mengine mfano wake.Anasema Ibnu Aqeel :"Na inachukiza kutawadha katika kisima ambacho kipo katika makaburi, na pia inachukiza kula matunda ya mti ambao uko kaburini kama vile mmea uliomea kwa mbolea ya najisi au mmea uliomea katika taka."
Na hii ndio kauli yakutegemewa kwa wanazuoni wa madhehebu ya Ahmad bin Hanbal, lakini kuhukumu yakwamba mchanga wa makaburini unabeba najisi hapo kuna angalizo , kwani najisi ikishabadilika kua mchanga hukmu yake pia inaondoka. Na hili linaungwa mkono na Hadithi iliyothibiti katika Sahihi mbili yakwamba msikiti wa Mtume ﷺ ulikua Makaburi ya washirikina na ndani yake kulikua na Mtende na jumba gofu Mtume ﷺ akaamrisha mtende ukatwe ukakatwa ukafanywa kibla ya waislamu ama jumba gofu akaamrisha likabomolewa, na pia akaamrisha Makaburi yafukuliwe , haya yalikua makaburi ya washirikina yaliofukuliwa na kutolewa zilizo kuwa ndani, kisha maiti yalivyofukuliwa mahala pale pakajengwa msikiti, pamoja na kubakia mchanga uliokua hapo, na lau mchanga ule wa makaburini ungekua ni Najisi basi ingekua lazima kuuondoa huo mchanga, kwa maana hii hii inamaanisha yakwamba mchanga huo ni tohara, na ikiwa Mchanga ni tohara basi na kila kinachomea katika Mchanga huo na kila maji yanayochimbuka katika mchanga huo pia ni tohara.
Na ALLAH ni mjuzi zaidi.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.