AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Hijra ya Kwanza Kwenda Abyssinia (Ethiopia):
Matukio dhidi ya Waislamu yalianza mwisho wa mwaka wa nane wa Utume, yalianza kidogo kidogo lakini baadaye yaliongeza kasi na kuwa mabaya kabisa. Jinsi siku zilivyozidi kwenda mbele hali ikawa ya kutisha na isiyovlimilika.
Ilipofika katikati ya mwaka wa tano, Waislamu walianza kulitafakari tatizo hilo kwa undani na kubuni njia muafaka za kuchukuliwa ill kukomesha utesaji huo. Katika wakati huo, uliojaa mashaka na kukata tamaa ndipo Suratil Kahf, sura ya kumi na nane, illposhuka ikiwa na majibu kwa maswali ya Mushirikina wa Makka waliokuwa wakimwuliza Mtume ﷺ mara kwa mara. Sura hiyo ina visa vitatu ambavyo ni pamoja na mafumbo ya kushawishi, kwa waumini wa kweli kupata maarifa.
Kisa cha vijana wa Pangoni kinaashiria Hijra, yaani kuondoka kwenye kitovu cha Dola ya Ukafiri na uadui ili kulinda Dini yao na kumtegemea Mwenyezi Mungu ﷻ:
وَإِذِ اعتَزَلتُموهُم وَما يَعبُدونَ إِلَّا اللَّـهَ فَأووا إِلَى الكَهفِ يَنشُر لَكُم رَبُّكُم مِن رَحمَتِهِ وَيُهَيِّئ لَكُم مِن أَمرِكُم مِرفَقًا} سورة الكهف:16}
[Na mkijitenga nao na vile wanavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, akufungulieni Mola wenu Mlezi rehema yake, na akutengenezeeni ya kukufaeni katika mambo yenu.] [18:16]
Kuna kisa kingine cha AI-Khidhr na Nabii Musa (Alayhi Salaam) kilicho wazi na ni marejeo nyetikwa mabadiliko maishani. Maisha ya baadaye ya mwanadamu si lazima yawe matokeo ya hali iliyopo, inawezekana kwa hakika ikawa kinyume chake. Kwa maneno mengine, vita walivyoponzwa Waislamu vinaweza vikawa na hali tofauti baadaye, na wakandamizaji makatili siku moja wakapata madhila na mateso ambayo yaliwapata Waislamu.
Zaidi ya haya kuna kisa cha Dhul Qirnain, kiongozi mwenye nguvu wa Magharibi na Mashariki. Kisa hiki kinaelezea wazi kuwa Allah ﷻ Huwapeleka watumishi Wake waadilifu kuutawala ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake. Aidha inaelezwa ya kuwa Allah ﷻ Huwateua watu waadilifu kila wakati ili kuwahami watu dhaifu dhidi ya wale wenye nguvu.
Suratul Zumar (sura ya 39) iliteremshwa kulizungumzia suala la Hijra moja kwa moja; na kueleza kuwa dunia ni pana sana inawatosha binadamu na Waumini wasijione kuwa wamebanwa na nguvu za mabavu na uovu.
لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۗ وَأَرْضُ اللَّهِ وَاسِعَةٌ ۗ إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ} الزمر:10}
[Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.] [39:10]*
* Arraheeq Al Makhtuum Uk 157-159
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.