AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Darul AI-Arqam:
Mtume ﷺ alipoona mateso ya kinyama yaliokuwa wakifanyiwa Waislamu yamekithiri, alifikiria ni busara kuwashauri wafuasi wake kuficha kusilimu kwao, kwa maneno na vitendo. Aliamua kukutana nao kwa siri ili Makuraishi wasijue mipango yake na hivyo kuchukuahatua ambazo zingeweza kuzuia kufikiwa malengo yake. Pia Mtume ﷺ alitaka kuepuka mapambano ya wazi na Mushirikina, kwa sababu kitendo hicho katika siku za mwanzo za ulinganiaji kisingesaidia - Imani mpya na changa yenye ulinganiaji kisingesaidia - Imani mpya na changa yenye kudhuriwa.
Siku moja katika mwaka wa nne wa Utume, Waislamu walipokuwa njiani kuelekea kwenye vilima vya Makka kuhudhuria mkutano wa siri na Mtume ﷺ, kundi la Mushirikina liliutuhumu msafara huo na kuanza kuwaghasi na kuwapiga.
Sa'd bin Abi Waqqas (Radhi za Allah ziwe juu yake) alimpiga Mushiriki mmoja na kumwaga damu yake na hili ndilo lililokuwa tukio la kwanza la umwagaji damu katika historia ya Uislamu.
Kwa upande mwengine, Mtume ﷺ alikuwa akitangaza Imani ya Uislamu na kuhubirl kwa wazi, kwa moyo mkunjufu na bidii, kwa maslahi ya mustakabali wa jamii na Waislamu wapya. Kwa kuzingatia stratejia ya kueneza Uislamu, aliamua kuanzisha kituo cha Kiislamu katika Dar AI-Arqam, nyumba iliopo katika milima vya Swafa.
Kituo hiki cha muda kilianzishwa mwaka wa tano kuanzia kupewa utume.*
* Arraheeq Al Makhtuum 157
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.