AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Miongoni mwa mbunu za Makuraish katika kumpinga Mtume Muhammad ﷺ ni:
3. Kuipinga Qur'an kuwa ni simulizi za watu wa kale, na kuwashughulisha watu kwa simulizi hizo, kwani imetajwa kuwa siku moja Al-Nadhir bin Al-Harthi alisema kuwaambia Makuraishi; " Enyi jamaa zangu, Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu ﷻ kwa hakika limewashukieni jambo na hamjapewa kutokana na jambo hilo hila, kwa hakika Muhammad . ni kijana mdogo mwenye kuridhiwa miongoni mwetu, mkweli sana kwa mazungumzo, anaongoza kwa uaminifu, mpaka mlipoona katika nywele zake zilizo kati ya jicho na sikio mvi, na amewajieni na yale ambayo amewajieni ndiyo sasa mnasema kuwa ni mchawi?'
"Hapana, Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu ﷻ yeye si mchawi, kwa hakika tumewaona wachawi na kuwapuuza na makuhani nao ni vivyo hivyo, kwani sisi tumekwisha kuona makuhani wangapi na kuvutiwa nao? Tumeyasikia maneno yake yaliyo na mpangilio maalumu ulio mzuri. Mkasema kuwa yeye ni mshairi, hapana, Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu ﷻ yeye si mshairi, maana tumesikia mashairi mengi na tumezisikia namna zake zote na tunafahamu bahari za mashairi ya Kiarabu mbalimbali."
"Mmesema ni mwendawazimu, hapana ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu ﷻ yeye si mwendawazimu, kwa hakika tumekwisha kuona wendawazimu wa kila aina, hakukuwa huku ni kukaba kwake na wala si kutia wasiwasi kwake, na wala si kuwadanganya kwake, Enyi jamaa zangu Makuraishi, chunguzeni katika jambo lenu, kwani kwa hakika kwa jinsi mambo yalivyo na hall ilivyo, Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu ﷻ, tumeshukiwa na jambo kubwa sana.
Baada ya hapo Al-Nadhr alikwenda mpaka Al-Hira na huko alikwenda kujifunza hadithi za wafalme wa Kifursi na hadithi za Rostom na Isfindiyar. Aliporejea ikawa ni kazi yake kusubiri Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ amalize kikao chochote cha kuwakumbusha watu kuhusu Mwenyezi Mungu ﷻ. Akiondoka tu, Al-Nadhri huvamia mahala hapo na kuanza kuwaeleza watu; Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu ﷻ, Muhammad si mzuri sana wa mazungumzo kuliko mimi, kisha huanza kuwahadithia kuhusu wafalme wa Faris na hadithi za Rostom na Isfindiyar, na kumalizia kwa kusema, ni kwa nini Muhammad awe mzuri zaidi kuliko mimi katika upigaji wa hadithi? (1)
Upokezi wa Ibn Abbas unafahamisha kuwa Al-Nadhr alikuwa amenunua waimbaji wa kike ambao alikuwa akiwatuma kwa kila aliyeelemea kwa Mtume ﷺ. Huko waliwalisha watu, wakawanywesha na kuwaimbia, kiasi cha kufanikiwa kuwalaghai, kusibaki kwao kuvutika kwenye Uislamu. Kwa huyo Al-Nadhr ilishuka Kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ Aliye Mtukufu:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّهِ} لقمان:6}
[Na miongoni mwa watu wapo wanao nunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu ... ] [31:6] (2) *
1) lbn Hisham, juzuu 1, Uk. 299, 358. Tafhimul Qur'an, juzuu .4, Uk. 8-9.
Mllkhtasar Sira Rrasul, Uk. 117-118. ,.
2) Tajhimul Qur'an, Juzuu 4, Uk. 9
* Arraheeq Al Makhtum Uk. 141
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.