AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Ibnu Ishaq amesema: 'Walikwenda watu kati ya watukufu wa Makuraishi kwa Abu Twalib, wakamweleza, Ewe Abu Twalib, hakika mtoto wa ndugu yako ametukana miungu yetu, ameitia dosari dini ye tu, ametupuuza na amewahusisha baba zetu na upotevu. Tunakuomba umzuie au tuachie tumshike, kwani kwa hakika hata wewe pia unaamini kile tunachokiamini sisi, kwa hiyo sisi tutakutenganisha naye.' Abu Twalib akawaeleza maneno laini, na kuwapoza hasira walizokuwa nazo, wakaondoka kutoka kwake na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ akaendelea kuidhihirisha Dini yake na kuwaita watu kwenye Dini hiyo.(1)
1 Ibn Hisham, Juzuu I, Uk. 265.
* Arraheeq Al Makhtum 132-133
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.