Menu

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


مختوم


Sauti ya ukweli haikuacha kuvuma katika pande zote za Makka, mpaka ilipoteremka kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ Aliye Mtukufu: 



{فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ}

 

[Basi (wewe) yatangaze uliyoamrishwa (wafa usijali upinzani wao) na ujitenge Mbali na (Vitendo 'Vya) hao washirikina.]   [15:94] 

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ akasimama na kuwaonya dhidi ya mambo ya ovyo ya kishirikina na upuuzi wake. Akawa anawabainishia ubaya wa masanamu na udhaifu wake, akawa akitoa mifano mingi, kuonyesha udhaifu wa hayo masanamu. Akawawekea wazi, kwa kuzitumia dalili zilizowazi, kuwa mwenye kuyaabudu masanamu, na akayafanya kuwa ni kiungo kati yake na Mwenyezi Mungu ﷻ  kwa hakika mtu huyo atakuwa katika upotevu ulio wazi. 

Watu wa Makka walighadhibishwa, walishangaa na kugutuka wakati waliposikia sauti inayodhihirisha ukweli, kuwakhofisha na upotevu, ushirikina na watu waliokuwa wakiabudu masanamu. Sauti yake ilifanana na sauti ya radi iliyoyavunja mawingu, ikatoa mweko na kulitetemesha anga lililokuwa tulivu. 

Makuraishi walisimama na kujiandaa kuyazima mageuzi na mapinduzi haya yaliyochomoza ghafla, kwa vile walipata khofu kuwa mageuzi haya yangeondosha mambo yao ya kuiga na yale ambayo waliyarithi. 

Makuraishi walisimama imara katika msimamo wao kwa sababu waliamini kuwa maana ya kuamini ni kuukanusha Uungu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ﷻ, na maana ya kuuamini Utume na siku ya mwisho ni kujisalimisha kikamilifu na kutegemeza mambo yote moja kwa moja kwa Mwenyewe Mwenyezi Mungu ﷻ na kuwa haingebaki kwao khiyari (uhuru) katika nafsi zao au mali zao, sembuse kwa watu wengine.


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

8355439
TodayToday555
Highest 09-30-2026 : 21356
US
Guests 30

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6ac8dec846f6b4212400921791549128
title_6ac8dec846fba16501273171791549128
title_6ac8dec8470066371725581791549128

NISHATI ZA OFISI

title_6ac8dec84755d19078841711791549128
title_6ac8dec8475aa5691801241791549128
title_6ac8dec8475f54227159931791549128 Add content here

HUDUMA MPYA

: 11 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

Go to top
UongofuUongofu.com