Menu

KWA BANU SA'AD


 b60


Siku hizo ilikuwa ni mazoea ya watu wa mijini katika Waarabu kuwatafutia watoto wao wanyonyeshaji wa mashambani ili kuwaepusha watoto wao na magonjwa ya mijini, ill iwe na nguvu miili yao, ikazane mishipa yao na waweze kukisema Kiarabu fasaha katika utoto wao.Abdul Muttwalib akamtafutia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu  wanyonyeshaji. Alimtaka mwanamke mmoja kutoka katika ukoo wa Saad bin Bakri, Halima binti Abi Dhuayb amnyonyeshe Mtume.Mume wa bibi huyu alikuwa ni Al- Harithi bin Abdil-Uzaa aliyekuwa akijulikana kwa jina la Abi Kabshah kutoka katika kabila hilo hilo.
Ndugu zake Mtume wa kunyonya kutoka kwa mama huyo ni, Abdallah bin Al-Harithi, Unaysah binti Al- Harithi Hadhafa au Sudhamah binti Al-Harithi (na huyu ndiye Al-Shaymaa na hili ndilo jina lililoeleweka zaidi mijini kuliko hata jina lake halisi) naye alikuwa ni mmoja kati ya waliokuwa wakimlea Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na Abu Sufyan bin Al-Harithi Bin Abdul Muttwalib, mtoto wa Ammi ya Mtume
Ammi ya Mtume Hamza Bin Abdul Muttwalib alikuwa amenyonyeshwa kwa Banu Saad bin Bakri, mama yake alimnyonyesha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu siku moja wakati akiwa kwa mama yake Halima. Kwa hivyo,Hamza alikuwa ni mshirika na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu katika kunyonya kwa sehemu mbili, sehemu ya Thuwayba na sehemu ya Al-Saadiyya.


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668015
TodayToday703
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 28

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_686694ca9b75916565373161751553226
title_686694ca9b83a8671383051751553226
title_686694ca9b91010505901751553226

NISHATI ZA OFISI

title_686694ca9ceca14034352851751553226
title_686694ca9cfa68478615741751553226
title_686694ca9d07e15764738281751553226 Add content here

HUDUMA MPYA

: 15 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com