Menu

MAANA YA SIRA NA FAIDA ZAKE


 1


Kwanza kabisa ni nini Maana ya SIRA ?

Sira ni fani inayojishughulisha kuelezea maisha ya Nabii Muhammad tangu kuzaliwa mpaka kufa kwake, ikiwa ni pamoja na malezi na makuzi yake, wasifu wake wa kimaumbile, tabia zake, harakati zake katika kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa ummah, mahusiano yake na watu na mataifa mbalimbali.

Pia sira inaelezea hali ya ulimwengu kijamii na kiitikadi kabla na baada ya kuja Nabii Muhammad, kadhalika inataja maisha na utawala wa Makhalifa waongofu baada ya Mtume .

 

MADHUMUNI NA FAIDA ZA SIRA

 

Fani ya Sira inalenga kumfahamisha Muislamu:

1. Taswira na mfumo mzima wa Uislamu unatolewa na kutafsiriwa na maisha ya Mtume ﷺ.

2. Maisha ya Mtume Muhammad ndio kigezo na mfano mwema wa kuigwa na kufuatwa ili kuweza kupata mafanikio Duniani na Akhera. Mwenyezi Mungu atuambia:

 

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيرًا}    الأحزاب:21}

 

[BILA SHAKA MNAO MFANO MWEMA KWA MTUME WA MWENYEZI MUNGU…] [33:21]

3. Muislamu apate katika maisha ya Mtume Muhammad kitu kitakachomsaidia kuifahamu Qur-ani kwani aya nyingi za Qur-ani zinafasiriwa na kuwekwa wazi na matukio yaliyotokea katika uhai wa Mtume.

4. Sira inaonyesha ni njia na mbinu zipi alizozitumia Mtume mpaka akaweza kuusimamisha Uislamu katika ulimwengu uliokuwa umefunikwa na kiza totoro cha ushirikina.

5. Sira inaonyesha ni jinsi gani Mtume alivyoyatatua matatizo na vikwazo mbalimbali vya ndani na nje alivyokumbana navyo katika kumfikisha ujumbe wa Allah kwa watu wote.
Hizi ni baadhi tu ya faida zinazopatikana katika kuisoma na kuifuata sira ya Bwana Mtume .


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6785142
TodayToday143
Highest 07-17-2025 : 4917
US
Guests 31

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68a952b9b751c6713458781755927225
title_68a952b9b760514911660261755927225
title_68a952b9b76f316474188071755927225

NISHATI ZA OFISI

title_68a952b9b8c8f15090971461755927225
title_68a952b9b8d7213283904381755927225
title_68a952b9b8e5b5790996361755927225 Add content here

HUDUMA MPYA

: 4 + 12 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com