MJUE MTUME WAKO
UTANGULIZI
Yeye ni Muhammad Ibn Abdullah Mtume Asie jua kusoma wala kuandika,Ametumwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wote ili awabashirie mema na awaonye na mabaya.yeye ni Mtume wa mwisho.
Mwenyezi Mungu Subhanahu wataala Amemtukuza kuliko Mitume yote kama alivyo uyukuza Umma wake kuliko Umma wa Mitume walio tangulia,Imani ya Mtu haikubaliki mpaka amuamini Mtume Muhammad ﷺ Kuwa ni Mtume wa Mungu na Mtume wa Mwisho.
Sheria yake imefuta sharia zote zilo kuja kabla yake,Mwenyezi Mungu Amefaradhisha kumpenda na kumtii,Sifa zake na Alama zake,zimekuja
Mwenyezi Mungu (S.A.) Asema:
الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِنْدَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالإِنجِيلِ يَأْمُرُهُمْ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنْ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمْ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمْ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالأَغْلالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ أُوْلَئِكَ هُمْ الْمُفْلِحُونَ الأعراف: 157
"Wale wanaomfuata Mtume Nabii asiyejua kusoma wala kuandika ambaye wanampata ameandikwa kwao katika Taurati na Injili,anawamrisha mema na anawakataza mabaya na anawahalalishia vizuri na anawaharamishia vibaya na anawaondolea mizigo yao na Minyoyoro ilikuwa juu yao,basi wale waliomuamini na kumhishimu na kumsaidia na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye hao ndi wenye kufaulu" [Al'Araaf: 157]
Amebashiriwa na Nabii Issa (A.S) kwa kuja kwake,Mwenyezi Mungu (S.A) Anasema:
وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِنْ بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ فَلَمَّا جَاءَهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَذَا سِحْرٌ مُبِينٌ سورة الصف :6
[Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri! " [Asswaf: 6]
Na Mayahudi na Manaswara (Wakiristo) walikuwa wanamjua kwa sifa zake.
Mwenyezi Mungu Anasema :
وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ مُصَدِّقٌ لِمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِنْ قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُمْ مَا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ فَلَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الْكَافِرِينَ البقرة:8
[Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao!] [ Al-Baqara: 89]
Pia imepokelewa kwa njia isiyo na shaka kutoka kwa manaswara kuhusu kupatika utajo wa Mtume Muhamamd ﷺ: katika vitabu vyao kama alivyo.na katika qisa cha Hiraql Mfalme wa Kirumi alipo Muliza Abuu Sufyani Mas'ala kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W) Kisha akasema kumuambia Abuu Sufyan
( فإن كان ما تقول حقاً، فسيملك موضع قدمي هاتين، وقد كنت أعلم أنه خارج، لم أكن أظن أنه منكم ] ( البخاري]
"Ikiwa hayo unayo sema ni kweli basi atakuja kumiliki hii sehemu nilio weka miguu yangu,na nilikuwa ni najua kuwa atatoka (Mtume) lakini sikudhani kuwa atatoka kwenu"
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.