HAMZA YUSUF
\
Hamza Yusuf alizaliwa, Mark Hanson, huko Walla Walla, jimbo la Washington Amerika, na baadaye wazazi wake wakahamia jimbo la California na walikuwa wafuasi wa Greek Othordox, na akasilimu mwaka wa 1977 akiwa na umri wa miaka kumi na saba [17] katika mji wa Santa Babra Carlifonia.
Na sababu ya kusilimu kwake ni kutokana na kuokoka na ajali mbaya ya gari,na baada ya hapo akataka kujua uhakika wa uhai na Mauti,na akanza kusoma vitabu mbali mbali na katika vitabu alivyo soma ni Qur'ani Tukufu, na baada ya kusilimu kwake, aliamua kuusoma Uislamu iliapate kuufahamu na kulingania watu katika dini.
Safari ya kutafuta Elimu
Baada ya kusilimu kwake aliacha masomo yake ya University baada yakuwa ni Mwaka wa Mwiho kumaliza masoma, lakini aliamua kusafri na kwenda kutafuta Elimu ya kisheria alisoma Somo la Fiqhi,katika Dola ya Emirati, na kuhifadhi Qur'ani katika Mji wa Madina Saudi Arabia, na akasoma lugha ya Kiarabu na Mashair katika nchi ya Algeria na Marocco, na kusoma somo la Tasawf Mauritania na pia mbali na elimu ya sharia ya kiislam, alisomea filosofia na elimu ya saikologia.
Na ndiye mmwamerika wa kwanza kufundisha katika chuo kikuu cha zamani, Al- Karaoine Fez, nchini Morocco.
Mapema mwaka 1990, Hamza Yusuf alianza kufundisha baadhi ya jumuiya za Waislamu katika San Francisco, na mwaka 1996 alianzisha Zaytuna Institute,Taasisi ya Sayansi ya Kiislamu katika California, na akawa mhadhiri katika chuo hiko.
Na Taasisi hiyo inachapisha Vitabu,na kuricodi Mihadhara ianayo zungumzia Matatizo na Masuala ya kisasa yanayowakabili Wamarekani.
Na Waamerika wengi wamesilimu kupitia Taasisi hiyo.
Sheikh Hamza pia ni mwandishi wa vitabu kadhaa, ikiwa ni pamoja: Sheria ya Jihad - elimu ya watoto katika zama za kisasa - ajenda ya mabadiliko ya hali yetu.
Baada ya matukio ya Septemba, alichaguliwa kama Mshauri wa Rais Bush katika Mambo yanayo husu Uislamu.
Na Hamza Yusuf ni Imam wa Santa Clara Masjid ulioko Bay area, na ni mkurugenzi wa Zaytuna Institute, na vile vile ni mwendesha kipindi cha reality TV chenye utazamaji wa takriban watu million themanini [80] .
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.