Menu

ALAMA ZA KUBALIGHI KISHERIA


 

SUALI: Ni zipi alama za kubalaghi kwa mtoto za kisheria?

JAWABU: Kubaleghe kwa mtoto ni kutoka katika marhala ya utotoni na kuwa ni mwenye kukalifishwa na sharia na kuanza kuhisabiwa analolifanya. Kubaleghe kuna alama za Kimaumbile amabo za dhihiri kwa msichna na mvulana. Wanachuoni wamezitaja alama zinazo shirikiana kwa msichana na mvulana na alama zinazo wahusu wasichana peke yao.

Ama alama zinazo shirikiana ni kama zifuatavyo:

Alama ya Kwanza: Ni kuota, kutokwa na manii kwa mfulana na kwa masichana sawa akiwa amelala au akiwa macho kama ilivyo kuja katika aya

Alama ya pili: Ni kumea nywele sehemu za siri, nyele zenye kunyolewa wala sio zile nywele khafifu.

Na dalili ya alama hii ni kama ilivyo pokelewa kutoka kwa Mtume: Alipotaka Saa'ad bin Muaadh awatole hukumu mayahudi wa wabani Quraydha walipo fanya khiyana na Saa'ad akatoa hukmu wauliwe wanaume walio shiriki vitani na kufanywa mateka wake zao na watoto wao. Mtume  aliamuru kuangaliwa wale watoto walio kuwa wameshiriki kwenye vita wangaliwe ikiwa wameota nywele sehemu za siri wauliwe na ikiwa bado basi waachiliwe.

Alama ya tatu: Mtoto kufika miaka kumi na tano kwa hisabu ya mwezi wa mtizamo. Kwa habari alioisimulia Ibnu Umar Radhi za Allah ziwe juu yake; alinikagua mimi Mtume  katika siku ya Uhud kwa ajili ya kupigana na mimi nikiwa na miaka kumi na nne hakuniruhusu na akankagua siku ya Khandaq nikiwa na miaka kumi na tano akaniruhusu.

Ama alama zinazo husu msichana ni alama mbili

Ya kwanza ni kutokwa na hedhi,kwa hadithi ya Mtume  alipo sema:

   لا يقبل الله صلاة الحائض إلا بخمار]      رواه الترمذي]

[Mwenyezi Mungu hakubali swala ya aile na hedhi (msichana alie baleghe) ila kwa mtandio]      [Impokelewa na Al-Ttirmidhiy.]

Na alama ya pili: Nikushika mimba kwa sabubu Mwenyezi Mungu amejalia kuwa mtoto hutokana na maji ya mama na maji ya baba.

Amasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka :

 

{خُلِقَ مِن مَّاءٍ دَافِقٍ  يَخْرُجُ مِن بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ}

 

"Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu."     [Al-Twariq:6-7]

Na alama hii huregelea katika ile alama ya kwanza nao ni kutokwa na manii tulio itaja mwanzo.

Na Allah ndie mjuzi zaidi.

 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487088
TodayToday194
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 45

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e53a2bd81c14195762271735283618
title_676e53a2bd9068499708331735283618
title_676e53a2bd9ea14918936671735283618

NISHATI ZA OFISI

title_676e53a2bef5d4821974411735283618
title_676e53a2c968610576995261735283618
title_676e53a2c978c14979965991735283618 Add content here

HUDUMA MPYA

: 12 + 2 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com