Menu

VIPI NATAMKINAISHA MUME WANGU ILI ASWALI SWALA YA ALFAJIRI?


 

 

Mwanamke Mmoja aliuliza

Swali: Vipi nitamkinaisha mume wangu aswali alafajiri??

Jawabu: Baada ya kumshukuru Allah subhanahu wata'alaa na kumtakia rehma na amani Mtume na maswahaba zake.

Katika wema mkubwa ambao mwanamke anafaa kumtendea mume wake ni kua na pupa kumsaidia kwenye kutekeleza amri za Mungu na kumsaidia kuepuka maasia, Na hii ni katika sifa za wanawake wenye imani, tunamuomba Allah akulipe kheri na akusaidie katika hili unalo litamani kumkinaisha mume wako aswali Alfajiri kwa hakika msaada wa Mungu ndio unao tafutwa kwenye mambo tunayo yataka tuyapate na kwenye mambo tusio yapenda atuepushie.

Tutakupa nyasia katika mambo haya
Jambo la Kwanza;
Taka msaada kwa Mwenyezi Mungu,kwani yeye ndie muweza wa kila kitu.
Jambo laPili;
Jaribu Umkumbushe Mungu wake na umkumbushe na Kifo na siku ya hisabu kiyama na utafute njia mzuri ya kumuelezea Kwa hakika udhaifu wa imani ni sababu ya uvivu katika twa'ah na kinyume chake vile vile kuzidi kwa imani ni sababu ya kua na hamu kwenye kumtii Mwenyezi Mungu.
Jambo la tatu;
Mkumbushe umuhimu wa swala ya alfajiri na umuhimu wa kuiswali kwa wakati wake ikiwa ni mtu wakuichelewesha kwa wakati wake na pia umkumbushe umuhimu wa kuihifadhi swala kwa jamaa ikiwa ni mtu wa kuacha jamaa.
Jambo la nne;
kumuogopesha na hatari ya mwenye kuacha swala,au kuipuuza na kutoswali kwa wakati wake,na kuwa zimekuja hadithi za kukemea kwa mtu mwenye kuichelewa Swala,na kuwa asie swali alfajiri ni katika alama za mtu Munafik. 
Jambo la tanu;
Yatakikana utumie kila sampuli ya njia za kumnasihi hivyo ni haraka kukubali naswaha na kuziskiza.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu akuwafikie juu ya hili na awaongoze waislamu katika mambo ya kheri

Na Allah ndie Mjuzi zaidi.


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6785499
TodayToday500
Highest 07-17-2025 : 4917
US
Guests 24

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68a98c24b0cf42966647381755941924
title_68a98c24b0de01300998931755941924
title_68a98c24b0ec4228282541755941924

NISHATI ZA OFISI

title_68a98c24b24f94856172211755941924
title_68a98c24b25ec20744091491755941924
title_68a98c24b26b89955552381755941924 Add content here

HUDUMA MPYA

: 4 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com